KAMPENI YA MASTABODA YAZIDI KUSHIKA KASI,WASHINDI NANE WAJINYAKULIA ZAWADI ZA KISIMUJANJA AWAMU YA KWANZA

  Masama Blog      
 MENEJA Mwandamizi wa Idara ya Kadi Benki ya NMB, Manfredy Kayala, akimkabidhi zawadi ya simu mpya aina ya Tecno Pop 2 dereva wa Bodaboda kituo cha Buguruni Rozana, Mohamed Abdallah, baada ya kuibuka mshindi wa kufanya miamala ya kibenki zaidi ya 200 kwa mwezi kulipwa nauli na abiria wake kwa kutumia huduma mpya ya Master Boda QR, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za washindi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Idara ya Bidhaa za Kadi, Lupia Matta na Mwenyekiti wa    Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es Salaam, Michael Massawe. 

KAMPENI ya MastaBoda imezidi kushika kasi kwa kungia hatua ya pili ya utoaji wa zawadi za Simujanja kwa washindi nane wa awamu ya kwanza kujishindia Simujanja 'smartphone'.

MastaBoda ni kampeni  inayoendeshwa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwaunganisha waendesha Bodaboda katika mfumo wa kibenki wa kupokea malipo kwa Mastercard QR kutoka  kwa wateja wa Benki ya NMB, Benki zilizounganishwa na Mastacard QR pamoja na mitandao ya simu iliyounganishwa na huduma ya Mastercard QR.

Zoezi hilo la utoaji wa zawadi limeendeshwa jana Makao Makuu ya NMB na Meneja Mwandamizi Idara ya Bidhaa za Kadi, Lupia Matta.

Matta amesema NMB imejipanga kuwafikia waendesha Bodaboda elfu 75 Tanzania nzima, kwa lengo la kulasimisha biashara ya usafiri wa Bodaboda.

"Tunaenda kufanya kundi la waendesha Bodaboda kuwa kundi maalum linaloheshimika katika nyanja ya usafirishaji."Kupitia MastaBoda waendesha Bodaboda wanaenda kunufaika na mifumo ya kifedha inayotolewa na benki yetu. " amesema Matta.

Aidha Matta amebainisha kuwa wataendelea kutoa zawadi za Simujanja kwa wshindi wanaofikisha miamala zaidi ya 200 kwa mwezi mmoja na wale wanaofikisha miamala 50 kwa wiki wataendelea kujishindia elfu 50, huku zawadi kubwa ya Bodaboda aina ya Boxer zikitarajiwa kutolewa kuanzia Januari 2020 kwa washindi watakao fikisha miamala 600.

Washindi nane walioibuka na Simujanja ni John Haonga (Mabibo), Abdallah Maulid (Morroco),  Florian Calestine (Rozana), Twalha Ally (Rozana),  Mohammed Abdallah (Rozana),  Ebenezer Elisha (Mwenge), Ladislaus Abel (Ubungo) na Adam Gunza (Mlimani).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/370Wblg
via
logoblog

Thanks for reading KAMPENI YA MASTABODA YAZIDI KUSHIKA KASI,WASHINDI NANE WAJINYAKULIA ZAWADI ZA KISIMUJANJA AWAMU YA KWANZA

Previous
« Prev Post