Ticker

10/recent/ticker-posts

JEZI YAMUONDOA DISMAS TEN UMENEJA YANGA, ASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii

Uongozi wa Klabu ya Yanga umemsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi Kaimu Meneja wa timu hiyo Dismas Tena baada ya kuwavalisha sare zisizo halali benchi la ufundi na wachezaji.

Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya habari na Mawasiliano Yanga leo.

Katika taarifa hiyo, inadaiwa Dismas aliwavalisha sare benchi la ufundi na wachezaji ambazo hazijatengenezwa na mdhamini wa Klabu hiyo GSM kwa mujibu wa mkataba.

Aidha, wamesema uongozi umeamua kumsimamisha kwenye majukumu yakr ya umeneja ili kupisha uchunguzi wa kina wa suala hilo na hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa kwa kila aliyehusika.

Uongozi wa Yanga umewaomba mashabiki na wanachama waendelee kununua bidhaa halali zinazotengenezwa na kusambazwa na mdhamini wao GSM ili kuhakikisha Yanga inaendelea kunufaika na nembo yake pamoja na matumizi ya nembo hiyo.

Pia, wanaomba radhi kwa mdhamini wao kwa kitendo kilichofanywa na Meneja wao na kuhakikisha hakitajirudia tena na wamewatahadharisha wote wanaotengeneza, kusambaza na kuuza bidhaa zenye nembo ya Yanga waache mara moja ili kuepuka kuchukuliwa hatua za Kisheria.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QyMyDI
via

Post a Comment

0 Comments