JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA LAMFUKUZA KAZI ASKARI WAKE NA KUMPANDISHA CHEO MWINGINE

  Masama Blog      
Kamanda Wa Polisi mkoa Wa Arusha Jonathan Shana akimvisha cheo kwa niaba ya Inspekta Jenarali Wa Polisi, Askari NCO No.E.6767 Sergeant Meshack na kuwa staff Sergeant wa Polisi kuanzia December 22 kwa kitendo cha kukataa rushwa ya shilingi milioni 10,000,000 kutoka kwa mwananchi aliyekuwa anafatilia kesi ya ndugu yake kwa lengo la kumaliza kesi yandugu yake ambayo alikuwa anaifatilia


Na Woinde Shizza , Globu ya Jamii - Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemfukuza kazi kwa fedheha askari wake wenye namba F.8683 PC paulo Edward Erasmo kwa kosa la kushawishi rushwa ya shilingi milioni 10 kwa watuhumiwa ili kumpatia askari sajenti Meshack Laiser aliyekuwa amewakamata watuhumiwa wawili wakiwa na Lori la Mafuta wakiuza mafuta mtaani kinyume cha sheria.

Aidha jeshi hilo kupitia Mkuu wa polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro leo amempandisha cheo askari mwenye namba E.6767 Sajenti Meshack Samson Laizer kuwa Staff Sajenti kwa kukataa rushwa ya Sh.milioni 10 kutoka kwa watuhumiwa

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, ACP Jonathan Shana amesema kuwa askari huyo amefukuzwa kazi rasmi kwa kosa hilo la kwenda kinyume na kiapo cha jeshi hilo kwa kujihusisha na suala la rushwa kinyume cha sheria.

Askari huyo wa polisi inadaiwa kushawishi na kupokea kiasi cha shilingi millioni 10 ili ampatie askari Meshack aliyekuwa amewakamata watuhumiwa wawili wa kampuni ya kuuza mafuta ya Oryx waliokuwa wakiuza mafuta mtaani bila kutoa lisiti na kuisababishia hasara serikali .

Inadaiwa kuwa baada ya kuwafikisha kituo cha polisi waliachiwa kwa dhamana na kuwasiliana na boss wao ambaye alikubali kutoa kiasi hicho cha fedha ili suala hilo liweze kumalizika bila kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo Meshack ambaye anadaiwa kuwa na mawasiliano na viongozi wa ngazi za juu ,alibaini mchezo huo mchafu na kuwasiliana na maofisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Arusha ambao waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata askari huyo akiwa katika hatua ya kupokea kiasi hicho cha fedha.

Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana kwa niaba ya IGP Sirro, amempandisha cheo askari Meshack Laizer kuwa staff Sajenti kutoka cheo cha sajenti kutokana na ujasiri wake wa kukataa rushwa kiasi cha sh,milioni 10.

Alisema kitendo cha kukataa rushwa ni cha kizalendo na kinapaswa kuigwa na askari wote wenye uzalendo na nchi yao

"Lakini mbali na kumpandisha cheo askari Mesharck ambaye alijiunga na jeshi hili Mei 8 mwaka 1992, pia IGP amemzawadia Sh.milioni moja kwa kukataa rushwa hiyo na kuletea sifa jeshi letu,"alisema Shana.

Alisema jeshi hilo linatoa onyo kali jwa askari wake au mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vyabrushwa kwa sababu halitamuacha salama.
Aidha alisema upelelezi utakapokamilika watuhumiwa hao akiwemo askari huyo watapelekwa nahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Q6iYoA
via
logoblog

Thanks for reading JESHI LA POLISI MKOA WA ARUSHA LAMFUKUZA KAZI ASKARI WAKE NA KUMPANDISHA CHEO MWINGINE

Previous
« Prev Post