JESHI LA POLISI ARUSHA LAMNASA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JIJI HUMO

  Masama Blog      
Na,Jusline Marco:Arusha

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kumkata mtuhumiwa wa mauaji ya muimbaji wa nyimbo za injili Merry Richald Mushi yaliyotokea Desemba 25 mwaka huu katika kijiji cha Kilinga Wilayani Arumeru.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Jonathan Shanna amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Moses Lataeli Palanjo wakati akijaribu kutoka.

Kamanda Shanna amesema kuwa mnamo tarehe 28 mwezi huu majira ya saa kumi na moja na nusu jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kutumia mbinu ya Dog Style ambayo ndiyo imeleta mafanikio ya kumnasa mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kumuhoji kwa muda mrefu alikiri kufanya mauaji hayo.

Ameongeza kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na mtego kabambe uliokuwa umewekwa na jeshi la Polisi ambapo mtuhumiwa alikamatwa katika maeneo ya  kijiji cha Elkibushing Kata ya Oltrument Tarafa ya Muklati Wilayani Arumeru akiwa njiani kuelekea mafichoni nchini Kenya.

"Tumemuhoji kwa kina na amekiri kufanya kitendo hicho cha kikatili lakini jeshi la polisi lilienda mbali zaidi kutaka kujua ni kwanini kafanya kitendo hicho ndipo mtuhumiwa alikiri kwa kusema ni shetani tu."Alisema Kamanda Shanna

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meru Ndg.Furahini Mungure amesema kuwa tukio hilo ni miongoni mwa tukio lililotoke kipindi cha nyuma katika familia hiyo ambapo ndugu wa mtuhumiwa huyo aliwaua wazazi wake kwa kuwachinja.

Aidha Ndg.Furahini ameitaka familia hiyo na jamii kwa ujumla kupitia matukio hayo kufuata utaratibu wa shughulikia matatizo hayo kwa njia ya kidini na hata kijamii kwa kuangalia wapi walikosea na kutengeneza kutokana na historia ilivyo ya familia hiyo kwa mambo waliyoyafanya huko nyuma ili kuweza kunusuri kizazi kilichopo.

Nao viongozi wa waimbaji wa nyimbo za Injili Nchini akiwemo rais wa Umoja wa wanamziki Tanzania Dkt.Donald Kisanga pamoja na Mlezi wa waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha  wamelishukuru jeshi la polisi kwa kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokifanya.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 alifanya mauaji hayo kwa kumpiga na shoka kichwa Merry Richard Mushi mwimbaji wa nyimbo za injili mwenye umri wa miaka 24 ambapo anatarajiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu shitaka linalomkabili ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mount meru.

Baadhi ya majirani wamedai kuwa mtuhumiwa aliyekuwa akiishi nyumba kwa marehemu eneo la Kwapole Wilayani humo na alimpeleka nyumbani kwao kwa lengo la kumtambulisha ambapo walikaa kwa wiki tatu kabla ya kutokea kwa tukio hilo Desemba 25.

"Wakiwa nyumbani kwa baba yake na mtuhumiwa,kulitokea kutoelewana baada ya mtuhumuwa kudai apatiwe funguo za chumba cha marehemu ili aende mara moja lakinu marehemu alimkatalia huku akidai kwamba anadaiwa kodi hivyo kitendo cha kuonekana hapo ingeleta usumbufu kwa mwenye nyumba.Alisema jirani huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe

Aliendelea kwa kusema kuwa majibu yale hayakumpendeza mtuhumiwa ambapo siku ya tukio wakati marehemu akiwaandalua chai alionekana kunoa Shoka na baadae aliingia nalo ndani na baada ya kumaliza kunywa chai alimuita marehemu katika chumba walichokuwa wakilala na kuanza kumshambulua kwa kumkata na shoka mara mbili sehemu za kichwani na kuoelekea kifo chake.

Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mtuhumiwa huyo mzee Lataeli Palangyo amesema kuwa awali hapakywa na ugomvi wowote na walitarajia kusheherejea vyema sikumuu ya Krisimas pamoja.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Jonathan Shanna akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha polisi Usa river
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali na viongozi wa waimbaji wa nyimbo za injili mbele ya kituo cha polisi Usa river Wilayani Arumeru
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZAAghW
via
logoblog

Thanks for reading JESHI LA POLISI ARUSHA LAMNASA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI JIJI HUMO

Previous
« Prev Post