IGP SIRRO AWAONYA WANAOENDELEA KUWANYANYASA WANAWAKE NA WATOTO BUNDA, MARA

  Masama Blog      
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonya watu wanaonyanyasa wanawake na watoto, kwa kuwasababisia vipigo na ukatili wa aina nyingine ambao ni kinyume cha sheria za nchi. 

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Bunda mkoani Mara, ujenzi uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani UNFPA pamoja na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto yaani CDF. 

Katika sherehe hizo za uzinduzi IGP Sirro amewataka wananchi kutumia ofisi hiyo ya Dawati la kijinsia na watoto ili kuendelea kukomesha vitendo vya ukatili sambamba na kuwataka wazazi kuwaendeleza kielimu watoto wao jambo ambalo litasaidia jamii kuwa na viongozi bora. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Lydia Bupilipili amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kuchukua hatua madhubuti hususani katika kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, ukatili, mimba za utotoni, ulawiti, na ubakaji 

Aidha, katika ziara yake mkoani Mara, IGP Sirro tayari amekwisha zindua jumla ya Ofisi nne za Dawati la Jinsia na Watoto hatua ambayo itarahisisha upatikanaji wa taarifa zinazoripotiwa kwenye madawati hayo kuhusiana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33ELAKu
via
logoblog

Thanks for reading IGP SIRRO AWAONYA WANAOENDELEA KUWANYANYASA WANAWAKE NA WATOTO BUNDA, MARA

Previous
« Prev Post