HII NDIYO SAFARI YA MWISHO YA MZEE NEKEMIA KAZIMOTO, AZIKWA NA MAELFU YA WATU NYUMBANI KWAO KARAGWE.

  Masama Blog      
Anaadika Abdullatif Yunus wa MichuziTV.

Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa Shirika la Saidia Wazee Tanzania (SAWATA) Mzee Nekemia Mussa Kazimoto, yamefanyika nyumbani katika makaburi ya Nyumbani kwao Kayanga Karagwe mnamo Tarehe 23 Desemba 2019 yakihudhuliwa na maelfu ya waombolezaji, Viongozi na Wageni kutoka ndani na nje ya Nchi.

Akitoa Salaam  za rambi rambi Kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (MB) amemuelezea Marehemu Nekemia kama Mzee aliyependa kujituma na kuchapa kazi kwa bidii, na hivyo akiwasihi wananchi kujifunza kupitia kifo cha Marehemu Kazimoto, kuacha alama ya kukumbukwa.

Marehemu Kazimoto ambaye amefariki akiwa na Umri wa miaka 82, kutokana na shinikizo la Damu, pamoja na mambo mengine aliyoyafanya katika enzi za uhai wake, atakumbukwa kama Mzee mwenye hekima na busara kwani amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa nchini ndani ikiwemo kuasisi na kuongoza kupigania haki na stahili za wazee wenzake hapa Nchini kupitia Shirika la Saidia Wazee Tanzania (SAWATA), na huku akitumia uwezo na weledi wake kupigania masilahi ya Wazee.

Marehemu ameacha Mjane mmoja na watoto 14, ambao wapo katika nafasi mbalimbali, huku maisha yake akiwa ameyaweka wazi katika Kitabu alichokiandika Mwenyewe kiitwacho "Maisha na Harakati za Kazimoto" kilichohaririwa na Mzee Mwenzake Pius Ngeze.


 Pichani ni Enzi za uhai wa Mzee Kazimoto Siku ambayo Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli alipomtembelea nyumbani kwake Kwa ajili ya kumjulia hali
 Pichani msafara wa Magari likiwemo gari lililobeba Mwili wa  Marehemu Mzee Nekemiah Kazimoto, ukiwasili nyumbani Omugakorongo Kayanga Karagwe, baada ya kutolewa Hospitali Nyakahanga.
 Pichani ni baadhi ya Wana Familia ya Marehemu Nekemiah Kazimoto wakionekana kufurahia maisha ya mpendwa wao aliyoyaishi Kwa kipindi cha Miaka 82, kwa kupiga picha ya Pamoja.
 Pichani ni Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa (MB) akitoa salaam zake Kwa Niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa salaam Kwa familia na waombolezaji nyumbani Kwa Marehemu Kazimoto.
 Pichani Mama Mjane wa marehemu Kazimoto, akiongoza familia na Watoto kuaga Mwili wa Mpendwa wao, wakati shughuli ya salaamu za mwisho nyumbani kwao Omugakorongo Karagwe.
 Pichani Jeneza lililobeba mwili Wa Mzee Nekemiah Kazimoto likishushwa taratibu kwenye kaburi kuashiria kuwa hiyo ndiyo safari ya mwisho, ikishuhudiwa na Viongozi wa Dini, Chama, Serikali na waombolezaji.
 Pichani ni Mjane wa Marehemu akisaidiwa kuweka udongo wakati wa mazishi kama ishara ya kuzika na kwamba hatomuona tena mpendwa wake Mzee Kazimoto.
 Pichani ni mashada ya Maua yakiwa tayari yamewekwa juu ya kaburi la Marehemu Kazimoto Mara baada ya mazishi, kuashiria kuhitimisha safari ya Mzee Nekemiah Kazimoto, Bwana alitoa na Bwana alitwaa" Michuzi Media Group tunaungana na familia kuwapeni Pole mlioguswa na Msiba huo.
 Pichani ni Watoto wa Marehemu Nekemiah Kazimoto, akionekana Madam Flora akitoa Shukrani za Familia na pembeni ni Madam Edith Kazimoto.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rvWtkL
via
logoblog

Thanks for reading HII NDIYO SAFARI YA MWISHO YA MZEE NEKEMIA KAZIMOTO, AZIKWA NA MAELFU YA WATU NYUMBANI KWAO KARAGWE.

Previous
« Prev Post