Ticker

10/recent/ticker-posts

DEREVA ZINGATIA,KANUNI,SHERIA,MICHORO YA ALAMA ZA BARABARANI ,ACHENI VISINGIZIO NA KUSEMA WATU WANATOA KAFARA


Ally Nurdin (mwenye kipaza sauti) ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma.



Na.Vero Ignatus.

Madereva wa magari ya abiria wameaswa kukagua magari yao kabla ya kuanza safari ,sambamba na kuzingatia sheria ,michoro,kanuni,na alama za usalama barabarani ili kuepusha mwendo kasi na kusababisha ajali,hivyo kupelekea kusingizia kwamba watu wanatoa kafara

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya elimu mawasiliano na habari kwa umma( RSA) Ally Nurdin ,kwamba katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka ,waangalie matumizi sahihi ya barabara wakizingatia kuwa ni kipindi cha mvua ,kwani tayari watu walishashuhudia ajali zilizogharimu uhai hata kusababisha vifo, majeraha makubwa na ulemavu wa kudumu.

Nurdin amewahusia wamiliki wa magari binafsi haswa madogo ,kuwa makini katika kipindi hiki ambacho ,wanakuwa safarini kuelekea katika mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka, kwani kuendesha gari mjini haiwapi fursa ya wao kuendesha safari ndefu hivyo ni bora wafute dereva

''Wenye magari madogo wengi wamekuwa wakisafiri na magari yao,kumiliki gari na kuendesha mjini haikupi kibali cha wewe kusafiri safari ndefu,safari ndefu inahitaji uzoefu wa kutosha,kama hujazoea kusafiri safari ndefu nashauri utafute dereva akuendesha''

Aidha amewataka wazazi wawapo safarini kuwafunga watoto mikanda pia wasiruhusu watoto wao kurukaruka na kucheza kwenye gari wakati wa safari jambo ambalo ni hatari

''Wote waliopo kwenye gari wafunge mkanda na tabia ya kuwaacha watoto kurukaruka na kucheza ndani ya gari ni wakati wa safari ni hatari,pia acheni tabia ya kujazana kwenye gari kisa huyu ni binamu ,sijui mtoto wa mjomba ,baba mdogo epukeni hilo''alisisitiza Ally

Pia ametoa wito kwa abiria kuwa makini wawapo safarini kwa kutokupokea chakula cha aina yeyote kwa abiria mwenzake asiyemfahamu ,kwani anaweza kupata madhara ya kiafya au kuibiwa.

Sambamba na hayo amewataka watembea kwa miguu pia kuzingatia alama na michoro ya barabarani nyakati nzote,na katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka waepuke kutumia vilevi kupita kiasi ambapo inaweza kuwapelekea kulala pembezoni mwa barabara na wao wakuwa chanzo kimojawapo cha ajali .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Zi1qdl
via

Post a Comment

0 Comments