Ticker

10/recent/ticker-posts

DC NDEJEMBI AKABIDHIWA VIFAA VYENYE THAMANI YA SH MILIONI 25 KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA

Charles James, Michuzi TV

KATIKA kukuza sekta ya elimu katika Wilaya ya Kongwa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Deo Ndejembi amekabidhi mabati, mbao na mawadati yenye thamani ya Sh Milioni 25 kwa Shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.

Vifaa hivyo vimetolewa kwa shule sita za wilaya ya Kongwa na Benki ya NMB ambapo wamemkabidhi DC Ndejembi huku wakisema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuihudumia jamii lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kuwatumikia watanzania.

Akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi, DC Ndejembi amesema vifaa hivyo vitatumika kumaliza changamoto iliyokuepo na kuahidi kuhakikisha anasimamia kila Shule kupata mgawo kwa unaotakiwa kwa usawa.

Amesema Wilaya ya Kongwa imekua ikifanya vizuri kwenye sekta ya elimu ambapo mwaka huu wanafunzi 5000 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2020 huku akijinasibu pia kufanya vizuri kwa matokeo ya kidato cha nne.

" Tunawapongeza NMB hakika mmetushika mkono, tuna uhaba wa vyumba 39 vya madarasa lakini kwa sapoti yenu hii ya mabati, mbao na madawati hakika tutapunguza changamoto iliyopo.

Milioni 25 mngeweza kuzifanyia jambo lolote lakini mmeamua kumuunga mkono Rais wetu Dk Magufuli kwa kurudisha mchango wenu kwenye jamii hasa kwenye sekta ya elimu. Niwaahidi kusimamia vifaa hivi katika kuzifikia Shule zote zilizolengwa na zitumike vizuri," Amesema DC Ndejembi.

Amezitaka Taasisi nyingine za kifedha kurudisha mchango wao kwenye jamii hasa katika sekta ya elimu, afya na majanga ambapo huwalenga moja kwa moja wananchi wetu ambao kimsingi ndio wateja wa Benki hizo.

Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi amesema kila mwaka wamekua wakitenga kiasi cha fedha kwenye faida yao kwa ajili ya kurudisha mchango wao kwenye jamii na mwaka huu wametenga kiasi cha Sh Bilioni moja ambazo watazipeleka kwenye sekta mbalimbali.

Amesema Wilaya ya Kongwa imenufaika na vifaa hivyo kutokana pia na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia huduma ya benki hiyo hivyo wakaona ni vema kutenga kiasi cha Sh Milioni 25 kwa ajili ya elimu ndani ya wilayani humo.

" NMB tumekua na kawaida ya kutoa mchango wetu kwenye jamii katika nyanja tofauti ikiwemo Elimu, Afya, Majanga na Elimu ya Fedha kwa wanafunzi. Hivyo niwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii ili kumtia moyo Mhe Rais Magufuli ambaye ama kwa hakika ameleta ukombozi kwenye sekta hii kwa kutoa elimu bila malipo.

Niwaombe wazazi na taasisi nyingine pia kuwa na uchungu na elimu kwa kutoa michango ili kupunguza changamoto ambazo zimekua zikijitokeza," Amesema Mlozi.

Kiasi hicho cha Sh 25 Milioni kimeenda kwa Shule sita ambapo Shule ya Msingi Kibaigwa imepata mabati ya Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Miembeni imepata madawati ya Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Chinangali imepata Sh Milioni Tano, Shule ya Msingi Muungano imepata Milioni 2.5
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza na wanafunzi, wazazi na walimu wakati wa hafla ya kukabidhi madawati, mbao na mabati yenye thamani ya Sh Milioni 25 kwa Shule sita za Wilaya hiyo. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB Kanda ya kati
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi (kulia) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya kati, Nsolo Mlozi ikiwa ni jitihada za benki hiyo kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dk John Magufuli katika kutoa elimu bila malipo.

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza na wanafunzi, wazazi na walimu wakati wa hafla ya kukabidhi madawati, mbao na mabati yenye thamani ya Sh Milioni 25 kwa Shule sita za Wilaya hiyo. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB Kanda ya kati
 Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa mbalimbali vya elimu wilayani Kongwa.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni wilayani Kongwa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Deo Ndejembi wakati wa kukabidhiwa kwa vifaa mbalimbali vya kukuza sekta ya elimu ndani ya Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali ikiwemo Mabati, Mbao na Madawati kutoka kwa Benki ya NMB kama sehemu ya mchango wao kwenye jamii. Kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Bw Nsolo Mlozi.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36QsgMl
via

Post a Comment

0 Comments