Ticker

10/recent/ticker-posts

DC KATAMBI AMALIZA CHANGAMOTO YA ABIRIA WALIOKWAMA NA TRENI KUTOKEA KIGOMA

Charles James, Michuzi TV

KUFUATIA abiria waliokua wakisafiri na Treni inayotoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam kukwama jijini Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi ameagiza abiria hao kurudishiwa nauli zao.

DC Katambi ametoa agizo hilo kwa Stesheni Meneja wa Dodoma, Bi Rose Ngauga ikiwa ni pamoja na kuwatafutia abiria hao mabasi yatakayowasafirisha hadi mwisho wa safari yao.

Akizungumza na abiria hao leo katika stesheni ya Dodoma, DC Katambi amesema Treni hiyo imekwama jijini hapa kutokana na mvua inayonyeesha ambapo maji na mchanga zimefunika sehemu ya reli katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.

Amewataka abiria hao kuwa wavumilivu na watulivu kwani changamoto yao ishafika mikono mwa Serikali ambapo inashughulikiwa ili waweze kuendelea na safari.

" Nafahamu wengine mnaenda Hospitali, wengine mnawahi biashara zenu lakini ndugu zangu suala la mvua haliletwi na TRC ni mpango wa Mungu lakini sisi kama Serikali ni jukumu letu kutatua changamoto za wananchi wetu.

Najua mpo abiria 648 hapa, hivyo nimeagiza mrudishiwe nauli zenu na pia nitaita wamiliki wa mabasi hapa waweze kutupa mabasi ya dharura kwa ajili ya kumalizia safari yenu.

Awali Stesheni Meneja, Rose Ngauga amesema tayari wataalamu wa Shirika la Reli wameshafika katika maeneo ambayo yamepata adha hiyo na wanaamini watatua changamoto hiyo ndani ya muda mfupi.

Kwa upande wake mmoja wa abiria Abdallah Sufiani ameishukuru serikali kwa kuingilia suala lao mapema na kulitatua kwa Mhe Mkuu wa Wilaya kuagiza warudishiwe nauli zao pamoja na kuagiza wapatiwe Chakula.
 Treni iliyokua ikitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam ikiwa imesimama katoka stesheni ya Dodoma baada ya kusimamishwa kuendelea na safari kufuatia sehemu ya reli katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro kujaa maji na mchanga na hivyo kuhatarisha usalama wa wasafiri.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi akizungumza na abiria waliokua wakisafiri na Treni inayotoka Mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam ambao wamekwama jijini Dodoma kufuatia mvua zinazoendelea kunyeesha
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mh Patrobas Katambi akizungumza na abiria wa Treni inayotoka Kigoma kwenda Dar as Salaam ambao wamekwama kutokana na mvua inayonyeesha ambapo maji na mchanga vimeziba njia katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro na hivyo kusababisha abiria hao kukwama katika stesheni ya Dodoma.

 Baadhi ya abiria waliokua wakisafiri na Treni kutoka Kigoma kwenda Dar as Salaam wakiwa nje ya Treni hiyo katika stesheni ya Dodoma ambapo imewalazimu Shirika la Reli nchini TRC kuwarudishia nauli na kuwatafutia mabasi ya kuwapeleka jijini Dar es Salaam ikiwa ni maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Q9rXXo
via

Post a Comment

0 Comments