DOWNLOAD APP YETU HAPA

DATA TAMASHA LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI UMUHIMU WA TAKWIMU NA TAARIFA

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KONGAMANO la kwanza kufanyika barani Afrika na kuwakutanisha   wanawake katika masuala ya data limefanyika leo katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam tawi Kijitonyama huku mlengo mkubwa ukiwa ni kujadili masuala ya wanawake ambapo tafiti zinaonesha kuwa asilimia 30 ya wanawake   pekee ndio wanaoshiriki katika masuala ya data jambo lililowapa  kiu ya kuwakutanisha vijana na wanawake waliofanya vizuri katika masomo hayo ili iwe chachu kwa vijana hao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Data Lab Stephen Chacha amesema kuwa leo wanasherehekea  taarifa na takwimu kupitia jukwaa la Data Tamasha ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali na baada ya hilo na wanaamini sera na maamuzi wanayoyafanya kupitia katika mifumo maalumu na kutoa taarifa sahihi za maendeleo kwa taifa hasa katika ujenzi wa taifa la viwanda.

Amesema kuwa tamasha hilo pia litajadili ushiriki wa wanawake katika masuala ya taarifa na takwimu na kwa namna zinasaidia katika  kufanya maamuzi, pia watajadili kuhusiana na uelewa wa wananchi katika masuala ya taarifa na takwimu na namna ya taarifa zinazowanufaisha wananchi kimaendeleo.

" Pia wadau kutoka nchi mbalimbali wapo na tutabadilishana uzoefu hasa kuhusiana na teknolojia katika ngazi mbalimbali na hiyo ni pamoja na kukuza uelewa kwa wananchi na kupokea taarifa zinazotoka kwa wananchi" ameeleza.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo kutoka Tanzania Data Lab   Mahadia Tunga amesema kuwa Data Lab imekuwa ikihimiza matumizi sahihi ya data katika kuleta tija katika maendeleo ya kiuchumi, na ameeleza kuwa data ni mkombozi katika jamii hasa katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na maendeleo zikiwa zimechakatwa kiutaalamu zaidi.

Amesema kuwa data imekuwa zimekua zikitatua changamoto kadha wa kadha katika taasisi za umma na binafsi na ameshauri taasisi hizo kuendeleza matumizi ya data kwa usahihi ili kuweza kutatua changamoto za aina hiyo.

"Katika biashara pia Kuna uhitaji mkubwa wa matumizi ya data, pia hata kwa wanafunzi wa Sekondari, Serikali na taasisi nyingine zinazoshughulikia masuala  ya kijamii ndani na nje ya nchi na ili  kuleta maendeleo data lazima zihusike" ameeleza.

Hafla hiyo ilienda sambamba na maonesho ya data katika nyanja mbalimbali yaliyooneshwa na wanafunzi kutoka Chuo kikuu Dar es Salaam wanaosomea masuala ya data.
 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Data Lab nchini Stephen Chacha Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana sherehe ya Data Tamasha ambapo ameeleza umuhimu wa data katika shughuli za kijamii ikiwemo utunzaji wa kumbukumbu zenye kusaidia jamii, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa mafunzo kutoka Tanzania Data Lab Mahadia Tunga akizungumza na waandishi kuhusiana na hafla hiyo ambapo ameeleza kuwa data husaidia sana katika kufanya maamuzi, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wakiwemo wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali katika sherehe za Data Tamasha lililofanyika katika Chuo kikuu Cha Dar es Salaam tawi la Kijitonyama, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Tamasha la Data Tamasha wakiwa katika picha ya pamoja.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2DH1eKO
via
logoblog

Thanks for reading DATA TAMASHA LAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI UMUHIMU WA TAKWIMU NA TAARIFA

Previous
« Prev Post