CHUO KIKUU CHAIBUKA KIDEDEA MKUTANO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU AFRIKA KUHUSU SHERIA

  Masama Blog      
Mshindi wa wa kwanza katika kipengele cha kujenga hoja wakati wa Mkutano wa Saba wa Mpango wa Mafunzo kwa Nchi za Maziwa Makuu katika masuala la Kimataifa ya Sheria za Kibinadamu na Haki za Binadamu; uliofanyika katika mji wa Kigali nchini Rwanda Bi. Hazel Karua akiwa katika picha ya pamoja na mshiriki mwenzake Bw. Jeofrey Ernest Lukwaro baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi. Mjadala kuhusu masuala la Sheria za kimataifa kuhusu masuala ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ukiendelea, Kigali Rwanda. Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Saba wa Mpango wa Mafunzo kwa Nchi za Maziwa Makuu katika masuala la Kimataifa ya Sheria za Kibinadamu na Haki za Binadamu; uliofanyika katika mji wa Kigali nchini Rwanda wakiendelea kufuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa. Baadhi ya Wanafunzi wawakilishi kutoka Tanzania wakishiriki mafunzo kuhusu Sheria za kimataifa za masuala ya Kibinadamu na Haki za Binadamu, Kigali Rwanda. Wakiwa kwenye picha ya pamoja, ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Deogratius Mapendo (Katikakati) pamoja na wanafunzi waliowakilisha Chuo Kikuu Mzumbe katika mashindano Bw. Jeofrey Ernest Lukwaro (kushoto) na Bi. Bi. Hazel Karua (kulia).


……………………………………………….

Chuo Kikuu Mzumbe kimeshiriki kwa mara nyingine Mkutano wa saba (7) wa Mpango wa Mafunzo kwa Nchi za Maziwa Makuu katika masuala la Kimataifa ya Sheria za Kibinadamu na Haki za Binadamu; uliofanyika katika mji wa Kigali nchini Rwanda.

Katika Mkutano huo Chuo Kikuu Mzumbe kimeibuka mshindi wa nne katika shindano la Mahakama ya kufundishia (Moot court) ambapo wanafunzi kutoka jumla ya Vyuo Vikuu 30 katika Ukanda wa Afrika vilishiriki, vikiwemo vyuo vingine vikuu vya Tanzania.

Nchi ya kwanza ilikuwa Kenya, ikifuatiwa na Uganda. Mzumbe iling’ara katika mkutano huo baada ya kuchukua zawadi nyingine ya kikombe kufuatia ushindi mwingine iliyopata kupitia mwanafunzi wake Bi. Hazel Karua kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Utetezi wa Hoja.

Mkutano huo umelenga kuwa na mikakati ya muda mrefu na mfupi katika kuimarisha Amani na utekelezaji wa Haki za Binadamu kwa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, kwa kutoa mafunzo na elimu inayohusu sheria za kimataifa katika masuala ya kibinadamu na Haki za Binadamu. (International Humanitarian Laws and Human Rights).

Wataalamu wabobevu katika masuala ya sheria za Kimataifa, Watetezi wa Haki za Binadamu kutoka Umoja wa Afrika, wataalamu wa masuala ya Wakimbizi na Watetezi wa haki za wazawa Afrika walipata fursa ya kuwasilisha mada ambazo zilijadiliwa.

Chuo Kikuu Mzumbe kiliwakilishwa na Mhadhiri Deogratius Mapendo kutoka Kitivo cha Sheria, pamoja na wanafunzi Jeofrey Ernest Lukwaro na Bi. Hazel Karua wote wa mwaka wa tatu kozi ya Sheria inayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sd0taj
via
logoblog

Thanks for reading CHUO KIKUU CHAIBUKA KIDEDEA MKUTANO WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU AFRIKA KUHUSU SHERIA

Previous
« Prev Post