Ticker

10/recent/ticker-posts

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LASHAURI NCHI WANACHAMA KUONGEZA VIFAA ZAIDI MIPAKANI ILI KUBAINI WAGONJWA WA EBOLA NA DENGUE


Na Mwandishi wetu Arusha.

Kamati ya mambo ya jamii katika Bunge la Afrika Mashariki imeshauri nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuhakikisha wanaboresha na kuongeza vifaa maalumu mipakani ili kuwabaini wagonjwa wa magonjwa ya milipuko kama vile homa ya Dengue na Ebola ili kuepusha kasi ya maambukizi baina ya nchi na nchi.

Aidha kamati hiyo ilitoa wito huo mapema jana kwenye bunge la nne la afrika mashariki linaloendelea jijini Arusha.

Akiongea na vyombo vya habari mapema jana mara baada ya kuwasilisha taarifa ya kamati hiyo ambayo ilihusisha nchi 3 mjumbe wa kamati hiyo bi Pamela Maassay,alisema kuwa wao kama kamati waliweza kutembelea nchi wanachama kwa ajili ya kukusanya na kujua mambo mbalimbali yahusuyo magonjwa hasa ya mlipuko.

Alidai kuwa katika mipaka ya nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki bado kunaitajika nguvu kubwa sana kwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ambazo wamekusanya wameweza kubaini kuwa zipo nchi ambazo wakati mwingine zinapata magonjwa kupitia Mipaka hivyo usalama unahitajika sana.

“Katika ripoti yetu tumeweza kuona nchi kama Rwanda ambayo kupitia mipaka yake ambayo ipo karibu na Kongo wamekuwa wakipata magonjwa sana kwa kuwa wapo karibu lakini tena kwa nchi kama Uganda nako hivyohivyo sasa taadhari inatakiwa ichukuliwe na kuimarishwa zaidi” aliongeza.

Katika hatua nyingine alisema hata kwa upande wa nchi ya Tanzania napo pamoja na kuwa kuna jitiada kubwa ambazo zimekwa kwenye mipaka lakini jitiada hata kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa ni muhimu sana.

“Kwa nchi nyingine magonjwa ya mlipuko tahadhari kubwa sana imechukuliwa kwenye mipaka wameweka vifaa maalumu ambavyo mtu akipita tu na ugonjwa anafahamika lakini pia hata kila zahanati ina jengo kabisa la wagonjwa hawa wa magonjwa ya milipuko tuige hili maana afya ya wananchi ni jukumu la kila kiongozi” aliongeza bi Pamela.

Alimalizia kwa kusema kuwa Wizara ya afya na maendeleo ya jamii hapa nchini iinatakiwa kuiga mfano huo kwa kujenga majengo lakini pia kuongeza vifaa mipakani kwa ajili ya kuepusha nchi na magonjwa hasa ya mlipuko yanayoweza Kutokea na kuathiri maisha ya wananchi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33SuMzU
via

Post a Comment

0 Comments