Ticker

10/recent/ticker-posts

BRELA YAWAKARIBISHA KWENYE MAONESHO YA VIWANDA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

WAKALA ya usajili wa biashara na leseni (BRELA) wanawakaribisha katika maoneshoya nne (4) ya Viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.

Akizungumza na michuzi Blog Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Loy Mhando amesema usajili wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma hataza pamoja na leseni za viwanda zinapatikana katika viwanja vya sabasaba ambapo maonesho ya bishara za viwanda yanafanyika.

Loy amesema leseni za biashara za kundi A nazo zinapatikana katika maonesho hayo hivyo wananchi wote wenye mpango wa kuanzisha biashara wafike katika viwanja hivyo ili wakapate huduma hiyo kwa urahisi zaidi na bila kupoteza muda.

"Natoa rai kwa watanzania wote, wadau wote wa biashara na viwanda pamoja na wawekezaji wanaohitaji huduma zinazotolewa na BRELA kufika katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kuangalia bidhaa zinazotengenezwa pamoja na kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa katika maonesho hayo". Amesema Loy.

Hata hivyo Afisa Leseni za viwanda kutoka BRELA, Yusuph Nakapala amesema kuwa katika maonesho hayo utapewa huduma ya kusajili biasha na jina la iashara kwa njia ya Mtandao.

AidhaNakapala amesema kuwa katika kusajili biashara au kiwanda kinacho hitajika ni kitambulisho cha NIDA na kama Kampuni ni mpya lazima uwe na namba ya  utambulisho wa mlipa kodi(TIN) kutoka TRA tuu utakuwa umesajili Biashara yako.

"Kwa upande wa raia wa kigeni kinachotakiwa katika kusajili wa kampuni au kiwanda ni hati ya kusafiria ya nchi husika na utakuwa umesajiliwa na mamlaka hiyo kwa njia ya kielektroniki". Amesema Nakapala.

Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA), Robertha Makinda amewakaribisha wananchi kwa ujumla katika maonesho ya Nne (4) ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaama kwa ajili ya kupata huduma zao na kupata elimu ya majukumu mbalimbali yanayofanywa na BRELA.

Wakala ya Usajili wa biashara na Leseni (BRELA) inawakaribisha wote Kutembelea Banda lao  la 105 lililopo katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa mtendaji Mkuu wa  Wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Loy Muhando akiwa na wafanyakazi wengine wakionesha jinsi mfumo wa zamani wa kusajili Biashara na majina ya biashara ilivyokuwa ikifanyika kwa njia ya kujaza fomu.
 Picha ya pamoja katika maonesho ya nne ya idhaa za viowanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Leseni za viwanda kutoka  wakala ya usajili wa biashara na leseni (BRELA), Yusuph Nakapala akizungumza na mteje aliyetembelea katika banda lao katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
 Mteja akipata maelekezo jinsi ya kusajili biashara katika maonesho ya viwana yanayoendelea katika viwanja vya saasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA), Robertha Makinda Katikati akizungumza katika maonesho ya viwanda yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2RuP5kr
via

Post a Comment

0 Comments