Ticker

10/recent/ticker-posts

Benki Ya Exim Yatoa Msaada Wa Taulo Za Kike Kwa Wanafunzi Wa Sekondari na Msingi Mkoani Shinyanga.

  Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 2,400 wa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo Mkoani Shinyanga.

Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama, Shule ya Msingi Mwenge, Shule ya Msingi Mapinduzi, Shule ya Msingi Jomu, Shule ya Msingi Ibadhi pamoja na Kituo cha Agape aids control Programme zilizopo mkoani humo.

Akizungumza wakati wa akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Meneja wa Benki hiyo tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul alisema hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares.

Alisema benki hiyo imekuja na mpango huo ili kusaidia wanafunzi wa kike kwa kuwapatia hitaji hilo muhimu kiafya sambamba na kutoa elimu kuhusu hedhi salama kwa wanafunzi wa kike pindi wakiwa shuleni.

Kwa mujibu wa Bi Sarah, kupitia mpango huo, benki hiyo inatarajia kutoa misaada mingine kama hiyo kwa shule kadhaa katika mikoa mingine ikiwemo Tabora na Iringa.

"Benki ya Exim inafarijika sana kuwa sehemu ya agenda muhimu za kijamii na hiyo ni moja ya imani yetu, kwa hiyo tumeamua kuja na mpango wa kusaidia mtoto wa kike na ili kuhakikisha kwamba msaada huu unakuwa na tija zaidi taulo hizi tulizotoa zinaweza kutumika zaidi ya mara moja na itawasaaidia zaidi wahusika,’’ alisema.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO inakadiriwa kuwa msichana mmoja kati ya kumi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara anakosa kwenda shule wakati wa mzunguko wa hedhi.

Aidha katika baadhi ya tamaduni suala la hedhi linapewa tafsiri potofu zaidi na hivyo kuongeza changamoto kwa watoto wa kike na hivyo kuathiri maudhulio yao mashuleni na hatimaye kuathiri taaluma zao.

"Benki ya Exim imejitolea kikamilifu kuhakikisha kuwa vijana wa Kitanzania wanapata elimu, licha ya changamoto zinazowakabili na hili tutalifanikisha kwa kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuwasaidia kuzitatua changamoto hizo na utoaji wa taulo hizi ni sehemu ya mkakati wa kukamilisha adhima hiyo,’’ alisema.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Istiqaama Bw Mbaraka Songoro alisema msaada huo kutoka benki ya Exim si tu unaonyesha utu bali pia ni unaonyesha heshima kwa watoto wa kike.

"Sisi kama shule tunaona hii kama heshima kubwa kwa wapokeaji wa msaada huu na kwa jamii kwa ujumla. Misaada ya namna hii inaonesha namna watu na taasisi makini kama Benki ya Exim zinavyowachukulia watoto wa kike…tunashukuru sana '' Alisema

Akitoa neno la shukrani kwa benki hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzie, Mwananfunzi Fathihiya Faiz, kidato cha tatu .kutoka Shule ya Sekondari Istiqaama.alisema mbali na uhitaji walio nao kwa bidhaa hiyo muhimu pia wameupokea msaada huo kama ishara ya upendo na heshima kutoka kwa benki hiyo hatua ambayo itawafanya wasome wakitambua kuwa zipo taasisi na watanzania wanaowajali na kutambua changamoto za kijinsia wanazopitia.

"Kwa msaada huu tunaamini hatutakabiliwa tena na magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa ukosefu wa taulo za hedhi. Pia msaada huu utaziba pengo ambalo wazazi wetu hawawezi kuliziba kwa sababu ya changamoto kadhaa zinazowakabili zikiwezo za kiuchumi,’’ alisema.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamopa na walimu pamoja na wanafunzi wa Kituo cha Agape aids control Programme kilichopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao kituo hicho mwishoni mwa wiki.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, wakiongozwa na Meneja wa Tawi hilo Bi Sarah Paul (katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaadawa taulo za kike kwa wanafunzi hao. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki
 Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Stella Malebetoh (Kulia) akifurahi pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi hao. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) wa benki hiyo unafahamika kama Exim Cares, iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Shinyanga, Bi Sarah Paul (Kushoto) akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa walimu wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Istiqaama iliyopo Mkoani Shinyanga ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule hiyo. Kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa kwa jamii (CSR) unaofahamika kama Exim Cares,  benki hiyo iliweza kutoa msaada taulo hizo kwenye shule sita zikiwemo za Msingi na Sekondari mkoani humo,mwishoni mwa wiki.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2q8KTeR
via

Post a Comment

0 Comments