Zaidi Ya Shilingi Bilioni Mbili Kukarabati Machinjio

  Masama Blog      
Na, Editha Edward-Tabora .

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora inatarajia Kutumia zaidi ya Shilingi bilioni mbili kufanya ukarabati mkubwa wa machinjio ya mifugo mjini Tabora baada ya kukamilisha nyaraka za upembuzi yakinifu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 

Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wametembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora na kuweza kujionea kile ambacho tayari walisomewa na wataalam kwenye nyaraka za upembuzi yakinifu ya kuomba fedha hivyo wa ajili ya ukarabati mkubwa wa machinjio hayo

Nae Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Joseph Kashushula amewaeleza Wajumbe wa kamati hiyo ya fedha hatua za mwanzo zilizotumika za kufanya ukarabati mdogo wa machinjio hiyo kuwa uligharimu zaidi ya shilingi milioni kumi na tano huku akisema mapato yatokanayo na tozo ya machinjio hiyo ambayo kwa siku inachinja kati ya ng'ombe sitini na tano hadi Sabini

"Tuna mipango mizuri ya kuhakikisha kwamba machinjio hii tunaikarabati na inakuwa ni ya kusasa zaidi tunategemea kupata pesa kutoka central government au kama itakuwa Siyo huko tutaweza kupata fedha kwa wafadhili na tayari maandiko tumeshaandika"Amesema Kashushula

Kwa upande wake Naibu meya wa manispaa ya Tabora Hahaha Muhamali amesisitiza umuhimu wa chanzo hicho cha mapato ya ndani ya halmashauri "sasa hivi tunatengeneza hizi kuta tunazowekea tailizi lakini hizi sakafu Siyo salama kiafya kwa Sababu nyama zinakaa chini haziko katika hali nzuri mimi nadhani tutajadili kwenye kikao chetu tutajadili tuone ni jinsi gani tuweze kufanyia ukarabati na hii sakafu"Amesema Muhamali 

Aidha machinjio hiyo ya manispaa ya Tabora imekuwa ikiingiza mapato ya wastani wa Shilingi milioni kumi na laki tano kwa mwezi kwa tozo ya uchinjaji wa ng'ombe pekee ukiachilia mbali na makusanyo ya tozo ya ushuru wa damu baada ya ng'ombe kuchinjwa.
Muonekano wa machinjio kwa ndani ambayo hapo awali yalikarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano. 
Wajumbe wa kamati ha fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakitembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora. 
Muonekano wa machinjio kwa ndani.
Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakiwa ndani ya machinjio hayo wakielekezwa jambo


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NahBF9
via
logoblog

Thanks for reading Zaidi Ya Shilingi Bilioni Mbili Kukarabati Machinjio

Previous
« Prev Post