WPP Scangroup yazindua mkutano, kuzungumzia mabadiliko ya kidigitali

  Masama Blog      
Mkurugenzi Mkuu wa Nala, Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever, David Minja, na Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications, Francis Majige katika mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup hivi karibuni.
Mkuu wa idara ya mikakati,Squad Digital, Parusha Partab akisikiliza katika Mkutano wa Reboot Tanzania iliandaliwa na WPP Scangroup.
Idriss Sultan, Omary Tambwe ( Lil Ommy) na Webiro Wassira (Wakazi) katika mkutano wa Reboot Tanzania iliyoandaliwa na WPP Scangroup hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya WPP Scangroup imezindua mkutano ya kwanza kuhusiana na mabadiliko ya kidigitali kwa lengo la kujadili mipango ya kuendeleza mazugumzo kuchochea mabadiliko ya kibiashara katika ulimwengu wa kidigitali.

Mkutano huo umezinduliwa leo na ni wa kwanza kufanyika nchini Tanzania, kwani kwa mara kwanza mkutano wa aina hiyo ulifanyika nchini Kenya mwaka 2018 na katika mkutano huo kampuni kubwa zinazojihusisha na ulimwengu wa kidigitali walipata nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Wakati wa mkutano huo wadau wametazama mazingira ya kibiashara na wameona kunamabadiliko makubwa na hasa kuongeza kwa watumiaji wa mtandao na mawasiliano.Kupitia mkutano huo imeelezwa kwamba kampuni ya WPP Scangroup mkakati wao ni kuwa kiongozi katika eneo la teknolojia na ubunifu.

Pia WPP Scangroup wamesema wanataka kuingiza toleo rahisi na bora ambalo lililobuniwa kwa lengo la kukamata fursa za soko zinazobadilika, na muundo ulioratibiwa uliojengwa na mahitaji ya wateja wao.

"Katika kuhakikisha tunafanikiwa katika ulimwengu wa kidigitali, tulifanya mkutano mdogo uliowakutanisha Mkurugenzi Mkuu wa Standard Chartered Bank Aljamair Riaz, Mkurugenzi Mkuu wa Nala Benji Fernandez, Mkurugenzi Mkuu wa Unilever David Minja na Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Communications Francis Majige Nanai,"imesema taarifa ya WPP Scagroup.

Katika mazugumzo yao Aljamair Riaz amesema kwamba kwasababu ya hali ya kidigitali kwa sasa, benki ya Standard Chartered wamebadilisha mkakati yao na kufuata upepo wa kidigitali. "Hapo mwanzo gharama ya ununuzi ilikuwa juu. Lakini tulivyo badilisha na kwenda kidigitali, tumeweza kuokoa fedha na kuwaongezea wateja katika bidhaa mbalimbali,"amesema.

Ameongeza kuwa huko Hong Kong wamezindua benki ya kidigitali tu ikiitwa ‘Virtual bank’. Pamoja na mambo mengine Kampuni ya WPP Scangroup katika kuhakikisha eneo hilo la digitali linapewa kipaumbele waliamua kuwaalika pia watu mashuhuri nchini ambao wako katika mabadiliko ya kidigitali.

Akizungumza katika mkutano huo Webiro Wassira ambaye anajulikana kama Wakazi amesema kama mtu mashuhuri ametoa maoni yake kuhusu nini kifanyike katika kuhakikisha digital inatumika kubadili maisha ya watu.

Wakati Omary Tambwe 'Lil Ommy' ambaye ni Mtangazaji wa Times FM aliyeshinda tuzo ya mtangazaji bora amesema kuna utofauti ya kuwa na followers wengi nak ujijengea brand.

Kwa upande wake Manish Sardana ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Squad Digital amesema kuwa ujio wa dijitali kumewafanya wao kama wafanyabiashara wanafikiria mikakati yao hasa linapokuja suala la matangazo wakati walengwa wengine wanafikiria tofauti kwa sababu ya uwepo wa hii ya media za kijamii."Hapa ndipo tunapoingia na kuamini kuwa ni muhimu kuwajulisha na kuelimisha washirika wetu wa biashara njia hii kupitia wakati huu wa ajabu."


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34OrbDD
via
logoblog

Thanks for reading WPP Scangroup yazindua mkutano, kuzungumzia mabadiliko ya kidigitali

Previous
« Prev Post