WAZIRI KABUDI ALIVYOWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS MAGUFULI KWA RAIS WA KENYA

  Masama Blog      
Mjumbe maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Uhuru Kenyatta juu ya masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Nchi hizo mbili na Kimataifa.

Katika Ujumbe huo Tanzania imesema itaiunga mkono Kenya katika nafasi ya Kiti na Mjumbe asiyewakudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2021/2022.

Mara baada ya kukabidhi na kueleza ujumbe wa Rais Dkt Magufuli kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyata,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepata fursa ya kushiriki katika uzinduzi wa ripoti ya Mpango wa kujenga umoja na mshikamano baina ya wakenya ujulikanao kama Building Bridge Initiative,ambapo amewataka wakenya kushikamana na kuziba mianya ya siasa za kikabila ili kuwa na Taifa moja kwa ajili ya maendeleo.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema Taifa hilo kwa miaka mingi limekuwa likiendeshwa wa siasa za kikabila jambo ambalo amesema halileti afya kwa ustawi wa Kenya kutokana na kuwa kila baada ya uchaguzi Taifa hilo huanza kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi badala ya kuzingatia masuala ya maendeleo.

Rais Kenyatta amewataka wanasiasa wenzake kuacha siasa zinazochochea mgawanyiko na kuwataka kutumia fursa iliyojitokeza kupitia Building Bridge initiative kutoa maoni ya namna bora ya kufanya siasa za kistaarabu zisizochochea uhasama.from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qIe4Wx
via
logoblog

Thanks for reading WAZIRI KABUDI ALIVYOWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS MAGUFULI KWA RAIS WA KENYA

Previous
« Prev Post