Ticker

10/recent/ticker-posts

WATOTO WAPATAO ELFU SITA WAISHI NA KUFANYA KAZI MITAANI NCHINI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiongea na wadau pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii mkoani Mwanza kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja kupambana na tatizo la watoto wa mitaani Jijini Mwanza.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katikati akifuatilia jambo pamoja na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ngondi kulia pamoja na Bw. Kizito Wambula kushoto ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wakifuatilia kwa Makini mada mojawapo kuhusu tatizo la watoto wa mitaani.


Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara aya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftali Ngondi akifafanua jambo kuhusu tatizo la watoto wa mitaani wakati wa kikao kazi kati ya Wizara na Wadau wa watoto Jijini Mwanza.


Wadau wa ustawi wa jamii, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Katibu Mkuu Wizara ya Afya na viongozi wengine Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha kupambana na tatizo la watoto wa mitaani Jijini Mwanza.

…………………


Anthony Ishengoma- Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wadau mkoani humo kwa kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa tatizo la watoto takribani 1,254 wanaoishi na kufanya kazi mitaani jijini Mwanza kwa kutumia mifumo na rasilimali zilizopo kumaliza kabisa tatizo hilo.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema lengo la kutaka kupunguza tatizo hilo sio la kuwaonea bali pia ni kuwasaidia watoto hao kuondoka na madhara na madhira wayapatao watoto hao ili waweze kurudi katika familia zao na kuondokana na maisha ya mashaka yanayowakabili.

Aidha Bw. Mongella amesema hayo leo Jijini Mwanza wakati wa Kikao Kazi cha wadau wa Mkoa wa Mwanza na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kilichokaa leo kujadili mpango Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani Nchini.

Bw. Mongella ameonya tabia ya baadhi ya taasisi na watu binafsi wanaotoa misaada kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao na kutaka kuwepo utaratibu wa kuangalia namna bora ya utoaji misaada hiyo mabayo amedai inachangia uwepo wa tatizo sugu la watoto wa mitaani.

‘’Unakuta mtoto anakuja mtaani na kupewa msaada unaotosha kwa wiki moja kwa msingi huu mtu huyu anazoea na kujenga tabia ya kutochukia maisha ya namna hii hivyo misaada hii inajenga usugu kwa baadhi ya watu hawa kutoona sababu ya kuachana na tabia ya kurudi au kendelea kuishi mitaani hivyo razima suala misaada liangaliwe upya.’’Alisisitiza Bw. Mongella.

Aidha kiongozi huyo wa Mkoa wa Mwanza ameongeza kuwa mkoa wa mwanza unaweza kutokomeza vitendo hivi kwa kuwa unayo mifumo mizuri ya ufuatiliaji kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa na kuwataka wadau mkoani humo kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha watoto hawa wanarudi katika familia zao na kuwafuatilia kupitia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

Wakati huo huo katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 iko wazi kwani inawataka watoto kuishi na kulelewa katika familia hivyo suala hili linaweza kutokomezwa kwa mjibu wa sheria hiyo.

Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa watoto hawa lazima warudishwe katika familia zao na uchambuzi ufanyike ili kubaini wale wote ambao hawataweza kurudi katika familia zao basi wapelekwe katika makao ya serikali ya wattoto ili waweze kupatiwa huduma bora ikiwemo chakula na maradhi.

Dkt. Jingu amewataka watoto hao kutambua kuwa wao ni azina ya Taifa hivyo wanatakiwa kuishi katika malezi bora na kuonya kuwa baadhi ya walezi kwa sasa ni waharifu na hivyo kuwafundisha watoto hao uharifu na kujiona wao sio sehemu ya jamii wanamoishi.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii hapa Nchini Dkt. Naftali Ngondi wakati akimkaribisha katibu Mkuu katika kikao kazi hicho amsema lengo la kikao kazi hicho ni kuja na mpango mkakati utakaowezesha kufuatilia utekelezaji wa kutokomeza swala la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kuisha kabisa kwa kuanzia na mkoa wa mwanza.

Aidha Dkt. Ngondi ameongeza kuwa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani nchini ni takribani elfu sita na kati ya hao asilimia tisini tayari wazazi na walezi wao wanatambulika hivyo kazi iliyopo ni kutafuta namna bora ya kuwaunganisha watoto hao na familia zao.

Wadau wa mashirika pamoja na wataalam wa ustawi wa jamii wanakutana jijini mwanza ili kukubaliana na kuja na mpango mkakati utakaowezesha utekelezji kwa vitendo namnan bora ya kuondokana na tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QnI1p5
via

Post a Comment

0 Comments