Ticker

10/recent/ticker-posts

Wananchi Tabora Wahimizwa Kushiriki Mbio Za Tabora Marathon


Na, Editha Edward-Tabora 

Wananchi Mkoana Tabora wehimizwa Kushiriki Mbio za TABORA GREEN MARATHON ili kuimarisha afaya zao sanjali na kutangaza vivutio vya ugali vilivyopo mkoani humo

Aggrey Mwanri mkuu wa mkoa wa Tabora mbele ya waandishi wa habari ameueleza uma kuwa Mbio hizo zitafanyika tarehe 30 novemba 2019 zitaqmbatana na upandaji miti na usafishaji wa mazingira katika kuleta dhana halisi ya GREEN MARATHON 

"Michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu hivyo wananchi mnatakiwa kujitokeza siku hiyo ili kuunga mkono Mbio hizi katika kuonesha ukakamavu na kuonesha mshikamano "Amesema Mwanri

James Makanza ni mratibu wa TABORA GREEN MARATHON amesema ni fahari kuwa na tukio hilo kwa mkoa huo wa Tabora ambapo litajumuisha viongozi mbalimbali na watu mashuhuri katika kuleta uhusiano mzuri ndani ya mkoa huo

Aidha mchezo huo wa riadha washiriki watakimbia umbali wa kilometa 2.5, 5,10, na Kilometa 15 ambapo zitaqmbatana na zawadi zikiwemo medali na utatolewa mti kwa ajili ya kuweka ishara ya Mbio hizo 
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na waandishi wa habari (pichanihawapo) kuhusiana na Mbio hizo za TABORA GREEN MARATHON.
Mratibu wa TABORA GREEN MARATHON James Makanza akizungumza kuhusiana na tukio hilo litakalofanyika tarehe 30 novemba 2019


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KiLqSj
via

Post a Comment

0 Comments