Ticker

10/recent/ticker-posts

WALIOKUTWA NA NOTI BANDIA ZA MIL 11WILAYA YA HAI, WAPANDISHWA KIZIMBANI.

Na Dixon Busagaga,Moshi

MFANYABIASHARA Chartone Mushi (44) na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, wakikabiliwa na makosa matatu likiwamo la utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh. milioni 11 ambazo ni noti bandia.

Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo namba 11 ya Uhujumu Uchumi ya Mwaka 2019 ni Richard Mtui (38) na Togolai Kingazi (34), wote wakazi wa Wilaya ya hai, mkoani Kilimanjaro.

Akisoma hati ya mashtaka jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bernazitha Maziku, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai mahakamani hapo kwamba Oktoba 19 mwaka huu huko katika maeneo ya Bomang’ombe, Wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro,

Washtakiwa hao Richard Mtui, Chartone Mushi na Togolai Kingazi, kwa makusudi waliunda genge la wahalifu na kundi hilo kutenda uhalifu wa kupokea na kusambaza noti bandia.

Katika hati hiyo ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa kinyume cha sheria na noti bandia zenye thamani ya Sh. milioni 11.

Wakili Mwinuka, alidai mahamani hapo kwamba kosa la tatu linalowakabili washtakiwa hao ni la utakatishaji wa fedha, ambalo ni kinyume na kifungu 3 (d), 12 (a) na 13 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2012,

Ikisomwa pamoja na aya ya 22 ya jedwali la kwanza la Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200 ya Sheria iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2002 na kifungu cha 16 cha sheria hiyo.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Maziku, alisema kwa kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana, washtakiwa wote watarejeshwa mahabusu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.





from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qDNrkQ
via

Post a Comment

0 Comments