Ticker

10/recent/ticker-posts

WAKAZI JAMII YA WAFUGAJI CHAMAKWEZA WAANZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI

NA MWAMVUA MWINYI, Chamakweza

WAKAZI jamii ya Wafugaji wa Kijiji cha Chamakweza Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze, Bagamoyo Pwani, wameanza ujenzi wa shule ya sekondari ambayo ikikamilika itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye shule mbalimbali.

Hatua hiyo itahamasisha baadhi ya jamii hiyo wanaoshindwa kusomesha watoto wao na wengine kushindwa kuwapeleka kwenye shule za Moreto na Chalinze ambazo ni za bweni na kutwa.

Wakizungumza kwenye eneo la ujenzi, Michael Kashina,
Lepa Mumbi na Solomon Madongo walisema ,ujenzi huo umeanza kutokana na juhudi za Lekope Langw'esi diwani wa Kata ya Pera, kata ambayo kwa sasa baadhi ya vijiji vyake vilivyokuwa katika kata hiyo vimehamishiwa Kata ya Vigwaza.

Kashina alieleza, katika harakati hizo wametumia shilingi milioni 13 kwa ajili ya kuweka bati kwenye vyumba vitatu na ofisi moja, ili wakipata ridhaa toka halmashauri waanze kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani, hatua inayopunguza msongamano katika shule zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.

"Langw'es akishirikiana na viongozi wenzake pamoja na wananchi walikaa kisha kuzungumza na mkazi aliyekuwa ameanza ujenzi wa sekondari binafsi, ambapo aliishia njiani ili awaachie majengo hayo yaliyopo ndani ya eka 50 kisha wampatie eneo mbadala"

Nae Mumbi alisema , miliki wa jengo hilo alilolenga kuwa sekondari ya binafsi, ameshindwa kulimalizia, hatua iliyowalazimu wao kumfuta wakamuomba ili wajenge shule ya Kata, kisha wao kumpatia eneo lingine lenye ukubwa wa eka 50 sawa na hilo. 

Diwani Langw'esi aliwashukuru wananchi wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wao kwa kukaa kisha kuibua mradi huo unaolenga kuwaondolea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.




from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34aLawI
via

Post a Comment

0 Comments