WADAU ZAIDI YA 300 WA KILIMO HAI WAPATA MATUMAINI MAKUBWA BAADA YA WIZARA YA KILIMO KUAHIDI KUSHIRIKI KIKAMILIFU...WATOA USHUHUDA

  Masama Blog      

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

WADAU wa kilimo hai zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya Tanzania wamekutana Jiini Dodoma katika Kongamano la Kimataifa la kilimo hai huku wengi wao wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelezwa kwa kilimo hicho baada ya Serikali kupitia Waziri wa Kilimo na  Chakula Japhet Hasunga kuelezea namna ambavyo Wizara hiyo itatoa kipaumbele kikubwa.

Wakizungumza leo katika Kongamano hilo la Kimataifa la Kilimo Hai , linaloendelea Mjini Dodoma, wadau hao wameiambia Michuzi Media Group kuwa wamefurahishwa na kauli ya Serikali iliyotolewa na Waziri Hasunga na kwamba wanaamini sasa kilimo hicho nitapata msukumo mkubwa nchini Tanzania.

Jana  wakati Waziri Hasunga anafungua kongamano hilo,amewaambia wadau wa kilimo hicho kuwa Serikali itaweka mkazo katika kuhakikisha Watanzania wanajihusisha nacho na katika sheria ya kilimo itakayokuja kilimo hicho kitakuwa na nguvu kisheria.

Mdau wa Kilimo Hai ambaye pia ni moja ya wajumbe wa Taasisi ya Kuelendeleza Kilimo Hai Tanzania(TOAM) Janeth Maro amesena  hakika wamefurahi kusikia sauti ya Serikali katika kushirikiana na wadau hao kukiendeleza kikamilifu na hiyo ni hatua kubwa yenye kuashiria kilimo hai kinakwenda mbele zaidi ya kilimo sasa.

Mkulima wa Kilimo Hai kutoka mkoani Morogoro Pendo Ndemo amesema ukweli uliopo kilimo hicho kinafaida kubwa ya kiuchumi na kiafya na kusisitiza kuwa wanaojihusisha na kilimo hai wengi wamefanya maendeleo makubwa.

 Ambapo amesema pia anajishughulisha na ugugaji na sasa anafuga kiasili  baada ya kupata elimu inayohusu kilimo hai."Nikuwa nafuga kiasili ,ninao ng'ombe wachache lakini wenye tija.Nimefanya maendeleo makubwa."

Wakati huo huo mkulima mwingine wa kilimo hai kutoka Masasi aliyejitambulisha kwa jina la Kuruthumu amesema amekuwa akijihusisha na kilimo hicho kwa miaka saba na kwamba amepiga hatua kubwa kimaendeleo na amekuwa akilima mazao mchanganyiko.

Kwa upande wake Mariam Kasambara amesema kwamba anajihusisha na kilimo hicho tangu mwaka 2012 huko mkoani Morogoro amesema kabla ya kuanza kilimo hai alikuwa mtumiaji mkubwa wa kilimo kinachotumia kemikali lakini baada alipata ushauri na kuanza kilimo hicho.

"Kilimo hai kwa kweli kwangu mimi nakiona kinafaa kwa mkakati hizo tulizonazo ni vema tukajikita katika kilimo hai .Magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa mangi yanachangiwa na ulaji mkubwa wa vyakula ambavyo vinatokana kemikali ambazo nyingi ziko kwenye mbolea, dawa za kuondoa wadudu.Njia pekee ya kuondoka na magonjwa ni kujikita katika kilimo hai,"amesema Paulini.

 Katika kongamano hilo pamoja na wakulima kutoa ushahidi  mzuri kuhusu kilimo hicho wamesisitiza ni vema Serikali ikaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo hicho kutatua changamoto zilizopo kwenye kilimo hicho.Hata hivyo Waziri wa Hasunga aliahidi kutatua changamoto hasa kwa kutambua vyakula vya kilimo hai ni salama zaidi.

Naye Albert Katagwira anayejihusisha na kilimo cha kahawa kinachotumia kilimo hai amesema anazo heka 150  za zao hilo na kwamba zao la kahawa ni la kimkakati na changamoto kubwa ilikuwa soko.

Hivyo baada ya kuona changamoto hizo aliamua kujikita katika kilimo hai na kwamba ametenga heka 50 na kuna tofauti kubwa hasa ya bei."Kahawa ninayo Lima mimi natumia kilimo hai, angalau nauza  vizuri kuliko wenzangu wanaolima kahawa kwa kilimo cha kisiasa,"amesema.

Amesema kutokana na kujikita na kilimo hicho msimu wa kilimo uliopita amechaguliwa kuwa mkulima Bora wa mwaka wa  kilimo cha kahawa na shamba lake la kahawa inatumika kama shamba darasa na kuna vyuo vingi wanafunzi wake wanakwenda kujifunza .Amesema hata mbolea anayotumia ni ya mabaki ya majani ya kahawa na mbolea ya samadi. 

Hata hivyo wadau wengine wamesema bado kuna changamoto ya kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu kilimo hai na kwamba kuna watu wanatamani kujua kwa kina  kuhusu kilimo hicho

Wakati Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ametumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kujengewa hoja zinazoshawishi kilimo hicho."Ninachokiona hapa wote tunaweza kujihusisha na kilimo hai lakini kuna mahali hatujaelewana jinsi ya kwenda pamoja kufikia kilimo hai."
Mbunge wa jumbo la  Chemba Juma Nkamia akichangia wakati wa kongamano la Kimataifa la Kilimo hai ambapo wadau zaidi ya 300 wakutana Mjini Dodoma kujadili mikakati ya kukiendeleza kilimo hicho.
Baadhi ya wadau wa kilimo hai wakifuatilia majadiliano ya kilimo hai yanayoendelea jijini Dodoma.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2DoLEmM
via
logoblog

Thanks for reading WADAU ZAIDI YA 300 WA KILIMO HAI WAPATA MATUMAINI MAKUBWA BAADA YA WIZARA YA KILIMO KUAHIDI KUSHIRIKI KIKAMILIFU...WATOA USHUHUDA

Previous
« Prev Post