Ticker

10/recent/ticker-posts

Vivalegacy yawakutanisha vijana katika kuweka suluhisho la ajira

Na Chalila Kibuda,Globu Jamii
VIJANA wameaswa kuwa na maarifa katika kujimarisha katika kufanya kuanzisha Kampuni au Biashara katika kutatua tatizo la ajira.

Hayo wameyasema wadau katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na Viva Legancy kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika masuala ajira katika kwa kuanzisha Kampuni au ujuzi wa kufanya ubunifu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu amesema serikali imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha vijana wanaondokana na changamoto ya ajira .

Amesema kuwa tatizo la ajira ni ukosefu wa maarifa hivyo vijana hao wakiwa na maarifa wataweza kuingia katika sekta ya Viwanda na kutatua tatizo la ajira.

Dkt.Semakafu amesema kuwa vijana wanatakiwa kufungua mawazo ajira badala ya kufikiria kuajiriwa.

Aidha amesema kuwa kumekuwa na mahusiano na sekta binafsi katika kuhusianisha masuala ya ajira ili vijana wengi waingie katika sekta hiyo kwa kuanzisha Kampuni na Biashara na kuweza kuajiri baadhi ya vijana.

Amesema kuwa ni wakati kuja pamoja kujipanga katika kuelekea uchumi wa kati kuhamasisha vijana kuingia katika uchumi katika kuanzisha Kampuni pamoja na Biashara.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Vivalegacy Fortunata Temu amesema kuwa kutakuwa na programu ya kutoa mafunzo ya vijana katika kuchimbua mawazo yao namna ya kufungua milango ya ajira kwa kuanzisha Kampuni au Biashara.

Amesema program za mafunzo zitakuwa kwa vijana namna ya kujiajiri.
Temu amesema kuwa vijana kwa pamoja wakiweza kutumia mafunzo hayo watafanikiwa ikiwa ni pamoja wanafunzi wa sekondari kuwaandaa kuhusiana na fursa za ajira.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye amesema kuwa wanaohitimu vijana kwa mwaka 1200,000 wanaoingia katika ajira ni 500000 hadi 600000 wengine wanakosa ambao hao wanatakiwa waingie sekta binafsi kwa kuanzisha Kampuni au Biashara.

Amesema kuwa waajiri katika nchi hii wachache ikilinganishwa na vijana wanaohitimu wanatakiwa kuajiriwa.

Simbeye amesema wakati mwingine sekta binafsi kwa vijana kuingia ni kutokana Mazingira ya kuwepo kwa tozo nyingi.

Hata hivyo amesema serikali inatakiwa kuwepo na sera kwa vijana wakianzisha Biashara kuacha kuchukua kodi ili waweze kuzalisha.
Naibu Katibu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  Dkt. Ave maria Semakafu akizungumza na waaandishi wa habari kuhusiana na kongamano la vijana kuhusiana na ajira lililoandaliwa na Viva legacy lilofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza katika kongamano la vijana kuhusiana na nafasi ya sekta binafsi katika kuweza kujiajiri katika kongamano lililoandaliwa na Viva Legacy jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Viva Legacy Furtunata Temu akizungumza namna walivyojipanga katika kutoa mafunzo kwa vijana katika kukabiliana na tatizo la ajira katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya vijana wakiwa katika kongamano lililoandaliwa na Viva Legacy jijini Dar es Salaam.

Naibu katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akifuatilia mda katika kongamano la vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33eYX4N
via

Post a Comment

0 Comments