Ticker

10/recent/ticker-posts

UBALOZI WA CHINA,TAASISI YA SUKOS KOVA FOAUNDATION WACHANGIA MRADI WA KUZUIA UJANGILI KANDO YA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI

Picha mbalimbali za Awamu ya Pili ya muendelezo wa mradi wa kuzuia ujangili katika vijiji vilivyopo kando kando ya hifadhi za Taifa nchini Tanzania. 

Mradi huu umefadhiliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania na kuratibiwa na Taasisi ya Sukos Kova Foundation. 

Awamu ya Pili ya mradi huu umehusisha msaada kwa wakazi wa kijiji cha Mhenda wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kijiji kilichopo kando kando ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Baadhi ya wanakijiji wa Mhenda hasa vijana hujihusisha na Ujangili kama njia ya kujiingizia kipato. 

Ubalozi wa China nchini Tanzania pamoja na Sukos Kova Foundation umewasilisha msaada  wa:

a) Mbegu za Mahindi - 2,500kgs
b) Mbegu za Alizeti - 1,500kgs
c) Mbegu za korosho- 800kgs 
Msaada huu unalenga kuwasaidia wanakijiji wa mhenda wapatao 3,000 kujishughulisha na kilimo badala ya ujangili kama njia ya kujiingizia kipato.

Aidha misaada mingine iliyotolewa ni:

d) Uniform - 13
e) Boots - 13 
Kama njia ya kuunga mkono juhudi za kikundi cha ulinzi shirikishi wilayani kisaki ambao ni wananchi wanaoshiriki kulinda hifadhi ya Taifa ya Mikumi. 

Pia Ubalozi wa China na Sukos Kova Foundation wamekabidhi Kompyuta pakata (Laptop) 4 pamoja na runinga 1 (TV set) kwa ajili ya kusaidia maafisa wa mikumi kuelimisha zaidi wakazi wa vijiji vilivyopo kando kando ya hifadhi hiyo kupinga ujangili na kuungana na Serikali katika kulinda na kutunza hifadhi hizo. 



 






from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34PPsJD
via

Post a Comment

0 Comments