Ticker

10/recent/ticker-posts

Tigo yazindua duka jipya Kigoma mjini

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akihakiki utendaji kazi wa mfumo wa kusajili namba za simu kwa alama za vidole katika duka jipya la Tigo lililopo eneo la Lubengela Mkoani Kigoma jana mara baada ya kuzindua duka hilo.Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati wa uzinduzi wa Duka la Tigo ‘Tigo Shop’ mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga akizungumza na wakazi wa Kigoma pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakati wa uzinduzi wa duka la Tigo Mkoani Kigoma, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati. 



Wateja wa Tigo Mkoani Kigoma wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya ‘Tigo Shop’ lililozinduliwa leo mkoani humo.

Duka hilo jipya litakuwa sehemu maalumu kwaajili ya wateja kujionea na kufanya majaribio ya bidhaa na huduma mbalimbali mpya na za kidigitali kama Tigo Pesa zitolewazo na kampuni hiyo.

Wateja pia wataweza kupata huduma ya kusajili upya namba za simu kwa mfumo wa alama za vidole.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema “Ufunguzi wa duka hili ni utekelezaji wa mkakati wa Tigo wa kufikisha huduma karibu na wateja na tunaamini kuwa duka hili litatoa fursa za biashara kwa wateja na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani hapa,” alisema Karembo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga aliipongeza Tigo kwa Kwa jitihada zake za kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye viwango vya kimataifa maeneo yote ya nchi.

“Duka hili jipya litakuwa chachu katika uboreshaji wa huduma za mawasiliano hapa mkoani Kigoma.Mkoa huu una wakazi wachapa kazi na wafanyabiashara ambao wanatamani kujikwamua kiuchumi hivyo hii ni fursa muhimu kwao,” alisema.

Aliongeza “Hii ni faraja kuona kwamba sasa huduma za Tigo zitapatikana kwa urahisi zaidi na hii itasaidia kufungua fursa nyingi za kiuchumi.”
Duka hilo linalopatikana katika mtaa wa Lubengela Kigoma Mjini, ni la kwanza mkoani humo na litakuwa likitoa huduma sambamba na dawati la wateja lililopo Wilayani Kasulu.

“Duka hili limewekwa katika eneo hili kimkakati ili kufikika kwa urahisi kwa wakazi wa Kigoma na maeneo jirani na mipakani,” alisema Madati.
Duka hilo linaifanya Tigo kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma zake maeneo mbalimbali ya nchi ili kufikia wateja wake zaidi ya 11.6 milioni jambo linalofungua milango kwa wateja kufurahia huduma za kidigitali zinazotolewa na kampuni hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37gsFbR
via

Post a Comment

0 Comments