Ticker

10/recent/ticker-posts

TAMISEMI Queens yaichapa JKT Mbweni na kutwaa ubingwa wa Muungano

Timu ya Mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI Queens) hii leo wamefanikiwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019 baada ya kuifunga timu ya JKT Mbweni magoli 40 kwa 23 katika mchezo wafainali wa michuano hiyo.

TAMISEMI Queens wamekabidhiwa kikombe cha ubingwa huo na kuweza kutoa pia mchezaji bora (MVP) na mchezaji bora wa katikati (center).

Akizungumza mara baada ya mchezo huo wa Fainali uliyofanyika katika Viwanja vya Gym Kana visiwani Zanzibar Mwalimu wa Timu ya TAMISEMI Queens Maimuna Rajabu Kitete amesema kuwa mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na wachezaji wake wameweza kufanya vizuri kutokana na alivyokuwa amewaandaa katika michuano hiyo.

“Wachezaji wangu niliwataka kucheza mpira na so kucheza na waamuzi wa mchezo ndo maana tuliweza kufanya vizuri katika mchezo waleo na kuibuka mabigwa wa michuano hii” ameeleza Mwalimu Kitete

Kwa kuongezea Mwalimu Kitete ametoa shukrani kwa Uongozi wa TAMISEMI,wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wao mpaka kufanikiwa  kutwaa ubigwa huu.

Mwalimu Kitete ameendelea kusema kuwa baada ya Ubingwa huu wanajipanga vizuri kuaangalia michuano ya Afrika mashariki inayokuja mbele yao baaada ya kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Muungano 2019

Lakini pia mchezo huo wa fainali timu ya JKT Mbweni walishindwa kucheza vizuri kutokana na wao kucheza na waamuzi wa mchezo huo kitu kilichowapa changamoto na kufanya kupoteza mchezo huo. 

Kwa upande mwingine zikiwa zimesalia dakika saba mchezo wa fainali hizo kumalizika timu ya JKT Mbweni waligomea mchezo na kutoka nje ya uwanja wakidai waamuzi wa mchezo huo kutokuwa sawa katika maamuzi huku timu ya TAMISEMI Queens wakibaki uwanjani mpaka dakika za mchezo huo kumalizika na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

TAMISEMI Queens ilikuwa kundi B ikiwa na timu za JKT Mbweni, Mafunzo ya Zanzibar, Eangle ya Dar es salaam, Makotopola ya Dodoma na Zimamoto ya Zanzibar na katika hatua ya makundi walipata kushinda michezo yote na kuingia hatua inayofata mpaka kufikia fainali na kuwa mabingwa wa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa TAMISEMI Queens ni timu pekee ya wizara kutokea Tanzania Bara iliyoshiriki michuano hii na kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Muungano Zanzibar 2019.
Kikosi cha Timu ya TAMISEMI Queens kikiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanikiwa kuichapa JKT Mbweni katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Muungano na kutwaa ubingwa huo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/333Kjwi
via

Post a Comment

0 Comments