TAASISI NNE ZATII AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUZITAKA KAMPUNI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUTOA GAWIO

  Masama Blog      
Watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wakionesha mfano wa hundi zao leo ambazo ni jumla ya shilingi bilioni 2.75, wakati wa hafla ya kuwasilisha gawio kwa Serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dodoma.


Na Benny Mwaipaja, Dodoma


SIKU moja baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa muda wa siku 60 kwa wenyeviti wa bodi na watendaji wa Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 pamoja na yale ambayo Serikali ina hisa kutoa gawio na michango yao kwenye mfuko Mkuu wa Serikali lasivyo wangepoteza nyadhifa zao, taasisi 4 zimetoa gawio na michango kwa Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma leo jioni

Taasisi zilizotoa gawio ni pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kimetoa shilingi bilioni 1 nukta 2, Shirika la Reli (TRC) Sh. bilioni 1, Shrika la Posta Tanzania (TPC) sh. milioni 350 na Mfuko wa SELF-Microfinance shilingi milioni 200 na kufanya jumla ya kiasi kilichopokelewa kuwa shilingi bilioni 2 nuta 75

Jana Mheshimiwa Rais Magufuli alipokea gawio na michango mbalimbali ya sh. trilioni 1.05 kutoka kwa Kampuni, taasisi na mashirika 79 kati ya 266 yaliyotakiwa kutoa gawio na michango hiyo huku taasisi 187 zikikwama kufanya hivyo.

Hatua ya taasisi hizo nne kutoa gawio na michango yao leo imefikisha gawio na michango iliyopokelewa na Serikali katika mwaka wa Fedha 2018/2019 kufikia sh. trilioni 1.325 huku kampuni 183 kukabiliwa na rungu la Waziri wa Fedha na Mipango kama hawatatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kuwataka watendaji na Bodi zao kutoa fedha za gawio na michango ndani ya siku 59 zilizobaki


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2XTTnD6
via
logoblog

Thanks for reading TAASISI NNE ZATII AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUZITAKA KAMPUNI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUTOA GAWIO

Previous
« Prev Post