Ticker

10/recent/ticker-posts

TAASISI 418 ZA UMMA ZAUNGANISHWA TANePS, OFISA MTENDAJI MKUU PPRA ATOA MWITO

JUMLA ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS).

Hayo yamesemwa Novemba 11,2019 jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Leonard Kapongo alipokuwa akielezea  utekelezaji wa magizo ya Waziri wa Fedha, Dk.Philip Mpango kuhusu mfumo wa TANePS.

Alisema wakat waziri anatoa maagizo hayo taasisi nunuzi zilizokuwa zimeunganishwa zilikuwa 303 huku jumla ya wataalam wa nunuzi na tehama wapatao 924 walikuwa wamepatiwa mafunzo.

"Kutokana na juhudi kubwa zilozofanyika hadi kufikia leo hii Novemba 11, 2019 jumla ya taasisi 418 zimeunganishwa huku idadi ya watalaam waliopatiwa mafunzo kutoka taasisi nunuzi wakifikia 1,600. Hii inamaanisha kuna ongezeko la taasisi 115 zilizounganishwa toka siku tuliyopewa maagizo Septemba 28 mwaka huu," amesema Kapongo.

Mhandisi Kapongo amefafanua utaratibu wanaotumia kwa sasa ni kuwa mara baada ya taasisi nunuzi kupatiwa mafunzo taasisi zao huunganishwa kwenye mfumo na taasisi hizo huagizwa na PPRA kuanza kuutumia mfumo wa TANePS kwa kuweka mipango yao ununuzi kama hatua ya awali.

Ameongeza baada ya hapo kuendelea na kutekeleza michakato yote ya ununuzi inayofuatia ikiwemo kuweka matangazo ya zabuni ili wazabuni waweze kushiriki kwa njia ya kieletroniki na kwamba kati ya taasisi 418 zilizounganishwa, taasisi 200 zimekwisha anza mfumo huo hadi leo kwa kuwasilisha mipango ya ununuzi ya mwaka yenye jumla ya zabuni 11,343 zenye thamani takribani shilingi Trilioni 11.3.

"Kwa zile taasisi za umma ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo huo, PPRA inatoa mwito kwa taasisi hizo kudhuria mafunzo maalum yakutumia mfumo huu yanayoendeshwa na PPRA.

Orodha ya taasisi hizo itawekwa kwenye tovuti ya PPRA yaani www.ppra.go.tz," amesema.

Mhandisi Kapongo amesisitiza awamu ya mwisho ya mafunzo itazihusisha taasisi hizo na yanatarajiwa kuanza Novemba 16 mwaka huu na kuendelea hadi kufikia wiki ya pili ya Desemba na matarajio yao baada ya kukamilika kwa awamu hiyo taasisi zote nunuzi zitakuwa zimeunganishwa kwenye mfumo wa TANePS.

Hata hivyo amesema kwa upande wa taasisi nunuzi ambazo zingependa kufanyiwa mafunzo maalum zinaweza kuwasilisha maombi PPRA kwa ajili ya kupatiwa maelekezo zaidi kuhusu taratibu za utoaji wa mafunzo hayo.

"Nirudie tena kutoa rai kwa wakuu wa taasisi nunuzi kuwa matimizi ya mfumo wa TANePS ni ya lazima kwa sababu ni takwa la kosheria na kanuni zake na sio suala la utashi wa taasisi. Hivyo sisi PPRA hatutaishia kutoa mafunzo na kuziunganisha tu kwenye mfumo taasisi nunuzi bali tutafuatilia kwa karibu kuhakikisha matumizi sahihi na kamilifu ya mfumo, hatutasita kuchukua hatua stahiki," amesema.

Aidha, ametoa mwito kwa watoa huduma mbalimbali, wazabuni na makandarasi wote nchini kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye michakato ya zabuni kwa kujisajili kwenye TANePS kupitia tovuti ya mfumo ambayo ni www.taneps.go.tz.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo huo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS) kwa Waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam,ambapo alisema kuwa  jumla ya Taasisi 418 zimeunganishwa kwemye Matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (TANePS) kati ya Taasisi 540.Pichani kulia ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James .
 Mwenyekiti wa Bodi  wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga akizungumza mbelee ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar,kwa kuishukuru Serikali kuanzisha mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambao utaongeza ufanisi zaidi ya Serikali na kuongeza zaidi pato la Taifa,na kuwaletea Wananchi maendeleo. 



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Kc9JB7
via

Post a Comment

0 Comments