Shabiki wa Simba asimulia alivyoshinda Mil 393 za M-Bet

  Masama Blog      
Mkazi wa mkoa wa Iringa, Salvatory Kambaulaya amejishindia kitita cha Sh 393,200,750 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-bet Tanzania.

Kambaulaya ambaye ni shabiki wa Simba na Manchester City alisema kuwa hakuwa na wasiwasi mara baada ya kupigiwa simu na Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa ni mshindi wa fedha hizo.

“Niliamini kuwa ni mshindi kwani mimi siyo mtu wa kwanza kushinda droo ya Perfect 12 ya M-Bet kutoka mkoa wa iringa, kuna mwanafunzi alishinda na kupatiwa fedha zake,

“Niamini M-Bet kwa kuwa na washindi wa uhakika katika michezo yao, ndiyo maana nilicheza ‘mikeka’ saba, mmoja nikipatia mechi tisa na mwingine mechi 12,” alisema Kambaulaya. Alisema kuwa kiasi cha fedha alichoshinda ni kikubwa sana na anatakiwa kutuliza akili ili kujua nini anafanya kwa upande wa maendeleo.

“Nimeshinda zawadi ya kwanza, lakini nimeumia sana na matokeo kati ya timu yangu, Manchester City ilipofungwa na Liverpool, niliweka Manchester kuwa ni washindi, hata hivyo alifungwa mchezo huo. Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa Kambaulaya ambaye ni afisa polisi mkoani Iringa ataweza kubadili maisha yake kupitia mchezo wao wa Perfect 12.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa ambao wamefaidika na msemu huo tokea kuanza kwa ubashiri. “Tumetoa washindi wengi mpaka sasa ambao wamejishindia mamilioni ya fedha na kuweza kubadili maisha yao ya kila siku,” alisema Mushi.
 Mshindi wa Sh milioni 393 wa mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Salvatory Kambaulaya ( wa pili kulia) akiwa kayika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania Allen Mushi (wa pili kushoto) mara baada ya kukabibidhiwa mfano wa hundi kwa kushinda kitita hicho cha fedha. Wengine katika picha ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubashiri na Kulia ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala. 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OqIkNn
via
logoblog

Thanks for reading Shabiki wa Simba asimulia alivyoshinda Mil 393 za M-Bet

Previous
« Prev Post