Ticker

10/recent/ticker-posts

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WANUNUZI WAKUBWA WA TANZANITE

Waziri wa Madini Doto Biteko akimzawadia mmoja wa Wanunuzi Wakubwa waMadini ya Tanzanite zawadi ya Kinyago cha Twiga. Wengine wanaoshuhudia niMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, Katibu Mkuu wa Madini Prof.Simon Msanjila na Mwenyekiti wa TAMIDA, Sam Mollel.
Waziri wa Madini wa Madini Doto Biteko akimkabidhi picha inayoonesha MlimaKilimanjaro mmoja wa Wanunuzi Wakubwa wa Madini ya Tanzanite. Wenginewanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, Katibu Mkuuwa Madini Prof. Simon Msanjila na Mwenyekiti wa TAMIDA, Sam Mollel.
Sehemu ya Ujumbe wa Wanunuzi Wakubwa wa Tanzanite wakifuatilia hafla yakuwaagwa kwao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa KIA.
Sehemu ya Maafisa wa Serikali wakiwemo Maafisa Madini waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri wa Madini Doto akimwonesha mmoja wa Wanunuzi wa tanzanite, Kitabu k cha Ramani kinachoonesha Madini yanayopatikana nchini kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

*************************************

Na Asteria Muhozya, Kilimanjaro

Serikali imewahakikishia Ushirikiano Wanunuzi Wakubwa wa Madini ya Tanzanite kutoka nchi za Marekani na Canada ambao Novemba 6, 2019, walihitimisha ziara ya siku tano nchini.

Ziara ya wanunuzi hao wakubwa ililenga kuona eneo ambalo madini hayo adhimu yanapozalishwa, kuona namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika, uzalishaji, uthamini, shughuli za uongezaji thamani madini hayo zinavyofanyika pamoja na masuala mengine yanayohusu madini ya tanzanite.

Akizungumza katika halfa fupi ya kuuaga ujumbe huo iliyofanyika katika Uwanjawa Ndege wa Kimataifa KIA, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa,ujumbe huo ndiyo wanunuzi wakubwa wa mwisho wa tanzanite yote dunianiambapo wananunua asilimia 75 hadi 80.

Ameongeza kwamba, wizara kwa upande wake imefurahishwa na ujio wa ujumbe huo kwa kuwa ni fursa ambayo itasaidia kutangaza madini ya tanzanite na mahali inapotoka na hivyo kuliwezesha taifa kupata wanunuzi zaidi wa tanzanite.

“ Tumepata watu wakubwa na wameahidi kuendelea kuja, hii itatusaidia kupatawanunuzi wazuri wa tanzanite, watatusaidia kutangaza madini yetu”.

Aidha, Waziri Biteko amesema Tanzania ndiyo mahali salama pa kuwekeza katika sekta ya madini na hivyo wizara kwa upande wake, inaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini ikiwemo wanunuzi wa tanzanite.

Pia, amekipongeza Chama Cha Wafanyabishara wa Madini ya Vito (TAMIDA) kwahatua hiyo ya kuwezesha wanunuzi hao kuja nchini na kueleza “TAMIDAmmethibitisha bila shaka mnaweza kufanya kazi na serikali’’.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel amesema kuwa ziara yawanunuzi hao ililenga katika kuitangaza Tanzania kama nchi pekee inayozalishamadini ya tanzanite duniani, kuona eneo ambalo madini hayo yanapozalishwa,ikiwemo kuona namna shughuli za uchimbaji wa madini hayo unavyofanywa ,uthamini unavyofanywa katika eneo la mirerani pamoja na udhibiti wa Tanzaniteunaofanywa na serikali.

‘’ Tumepata watu watakao simama na sisi kutangaza madini ya tanzanite, sualaambalo litawezesha pia bei ya tanzanite kupanda. Hata wao wanataka yasipite kwingine yakishaongezwa thamani hapa yaende moja kwa moja kwao.’’amesema Mollel.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo, Ken Oschipok kutoka kampuni ya
Diamond International amesema ni mara yake ya kwanza kufika Afrika na
amevutiwa na mazingira yote kuhusu tanzanite, ukarimu wa watanzania na
mazingira ya kibiashara na hivyo kuahidi kutumia fursa hiyo kutoa elimu kuhusuMadini hayo na uhalisia wake kwa watu wengine.

Mbali ya kutembelea migodi ya tanzanite Mirerani na kujionea shughuli za
uzalishaji wa madini hayo, pia, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea vivutiovya utalii vilivyoko nchini.

Aidha, hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna
Mhugwila, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mkurugenziwa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi na viongozi waandamizi wa Uwanja wa KIA.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36Ggc11
via

Post a Comment

0 Comments