SERIKALI YASEMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2019 UKO PALEPALE...KAMPENI KUANZA RASMI KESHO HADI NOVEMBA 23 

  Masama Blog      
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga akizungumza na waandishi wa habari leo wakati walipotangaza msimamo wa serikali kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji ambapo Kampeni zinatarajiwa kuwanza kesho.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga alipokuwa akizungumza nao leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo akizungumza na waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam wakati alipotangaza msimamo wa chama hicho kushiriki uchaguzi huo amesema chama hicho kinashiriki kikamilifu, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change ADC Bw. Doyo Hassan Doyo Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga wakiwa katika picha ya pamoja na wagombea wao wanaoshiriki katika nyazifa mbalimbali za uchaguzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa ADC Bi. Queen Sendiga akizungumza na kusisitiza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya wagombea wa chama cha Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) wameenguliwa katika uchagzui huo kwa makosa mbalimbali ya kikanuni na kisheria.
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akizungumzzia kuhusu makosa mbaimbali ambayo wagombe wa chama chake walifanya na kisha kuengeuliwa kikanuni na wasimamizi wa uchaguzi.
Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu yao yaliyopo Tandika wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

……………………………………………………….

SERIKALI YASEMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2019 UKO PALEPALE...KAMPENI KUANZA RASMI KESHO HADI NOVEMBA 23 


*Vyama vya siasa ambavyo vitashiriki vyatakiwa kupeleka ratiba ya mikutano ya kampeni Polisi wapewe ulinzi

*Watakiwa kufanya kampeni za kistaarabu katika maeneo yote, wagombea 12319 wapita bila kupingwa

Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

SERIKALI imeweka wazi kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka 2019 uko pale pale huku ikitangaza kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi huo zikitarajiwa kuanza kesho. 

Hivyo vyama vyote ambavyo vitashiriki uchaguzi huo zimetakiwa kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni kwa wakuu wa Polisi wa Wilaya kwa lengo la kupatiwa ulinzi kuhakikisha kampeni hizo zinakuwa salama na wagombea kupata fursa ya kujinadi kwa wapiga kura.

Wakati Serikali ikitoa msimamo huo baadhi ya vyama kadhaa vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Chama cha Wananchi(CUF) ,Chama cha ACT Wazalendo , Chama cha Chauma na NCCR Mageuzi wao walishatangaza kujitokea ,huku Chama Cha Mapinduzi(CCM) na vyama kadhaa vya upinzani vimetangaza kutoshiriki.

Akizungumza leo Novemba 16,mwaka 2019 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Nyamuhanga amesisitiza uchaguzi huo utafanyika kama ambavyo imepangwa na kampeni itaanza kesho nchini na kila kitu kiko sawa.

Amefafanua kuwa kwamba Watanzania waajiandae kusikiliza mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa na kisha Novemba 24 wakachague viongozi wao .Tunaomba vyama ambavyo vitashiriki kujiandaa na kampeni ambazo zinaanza kesho( leo) , ushauri wetu kwa vyama hivyo ni kupeleka ratiba ya mikutano yao ya kampeni za uchaguzi huu kwa wakuu wa polisi wa wilaya ili wapatiwe ulinzi,”alisema.

Kuhusu kampeni za uchagzi huo, ameeleza kuwa baada ya kuanza kesho,zitahitimishwa Novemba 23 mwaka huu ambayo itakuwa siku moja kabla ya upigaji wa kura kwa vyama vyote ambavyo vimebakia katika uchaguzi huo.Amesisitiza hakuna sababu ya uchaguzi huo kuusogeza mbele wala kuuahirisha.

Ameongeza kuwa kampeni za uchaguzi huo zinazoanza kesho zitafanyika katika maeneo yenye wagombea pekee na kuyaacha maeneo ambayo wagombea wake wamejitoa au kupita bila kupingwa jambo ambalo pia limevifanya vituo vya uchaguzi kupungua kwa kiwango fulani kutoka vituo 1,10000.

Nyamuhanga amesema kwa ujumla wagombea waliopita bila kupingwa katika mchakato wa uchaguzi huo nchi nzima ni 1,2319 sawa na asilimia 55 ya wagombea wote waliokuwa wamejitokeza kuomba kuteuliwa huku akitoa msisitizo kwa vyama vyote kufanya kampeni za kistaarabu.
Amesisitiza kuwa Wasimamizi wa uchaguzi, askari Polisi, mgambo wote wanapaswa kuwa katika sare kipindi chote cha kampeni hadi uchaguzi utakapofanyika ili kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza huku akitoa onyo kwa vyama hivyo na kuvitaka kuacha kutumia vikundi vya sungusungu na vinginevyo na kwamba sheria itachukua mkondo wake pale ambapo agizo hilo utekelezaji wake utakiukwa.

Katibu Mkuu Nyamuhanga amesema maandalizi ya uchaguzi huo yameshakamilika ikiwemo wino maalumu utakapakwa kidoleni mara baada ya kupiga kura pamoja na rakiri itakayotumika kufungia masanduku mara baada ya kuhitimishwa kwa zoezi la kupiga kura.

Wakati Serikali ikisisitiza kufanya uchaguzi huo, vyama vya ‘Alliance For Democratic Change’ (ADC) pamoja na Chama cha ‘Alliance For Africa Farmers Party’ (AAFP) vimetangaza kushiriki uchaguzi huo kwa kudai havioni sababu yoyote ya wao kujitoa.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Vyama vya Tanzania Labour Party(TLP) na chama cha National Reconstruction Party (NRA) kutangaza kushiriki mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa vikidai kuwa kufanya hivyo ni kuitendea haki demokrasia iliyopo nchini.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo amesema Chama chao kitashiriki uchaguzi huo licha ya ‘figisu figisu’ zilizojitokeza zilizosababisha baadhi ya wagombea wake kukosa kuenguliwa huku akikiri kuwa baadhi yao ‘walijichanganya’ katika mchakato wa ujazaji fomu za uteuzi.

Amesema ni kweli wapo waliofanya makosa ya aina mbalimbali katika ujazaji fomu hatua iliyosababisha kukiuka kanuni, kilichosababisha hayo kutokea hatuwezi kukilaumu kwa kuwa mengine yalitokana na uzembe wao kwa kutowapa elimu wagombea wao kabla ya kuzijaza fomu hizo.

Wakati Katibu Mkuu wa AAFP Rashid Rai, pamoja na kusisitiza kushiriki katika uchaguzi huo, amesema changamoto iliyojitokeza katika chama chake na kusababisha wagombea wake kuenguliwa ni kukiuka kanuni katika ujazaji fomu.

Hata hivyo amesema licha ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali wao bado watashiriki katika uchaguzi huo kwa kuwa bado wanao wagombea katika baadhi ya maeneo nchini.'Kwetu hata tukipata mtaa mmoja ni ushindi wa zaidi ya asilimia hamsini, haijarishi wenzetu wameshinda viti vingapi,"ameongeza.

Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ulioanza Oktoba mwaka huu kwa mchakato wa uandikishaji wapiga kura na baadae uchukuaji fomu, urejeshaji wa fomu, ukataji rufaa na sasa.kuanza kwa kampeni ambazo zitahimitishwa kwa kufanyika uchaguzi huo Novemba 24 kwa wananchi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/359ApdX
via
logoblog

Thanks for reading SERIKALI YASEMA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA MWAKA 2019 UKO PALEPALE...KAMPENI KUANZA RASMI KESHO HADI NOVEMBA 23 

Previous
« Prev Post