Ticker

10/recent/ticker-posts

SERIKALI YAOKOA BILIONI 34 /- KWA KUTUMIA MFUMO WA UNUNUZI KWA NJIA YA KIELETRONIKI-KATIBU MKUU

SERIKALI imesema imeokoa wastani wa Sh.bilioni 34 katika miaka mitano ya kwanza kutokana na kutumia mfumo  wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 11,2019,  Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali Doto James amesema kwa kuzingatia mfumo huo imeiagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu kuwa taasisi zote za ununuzi nchini ziwe zimeungwa katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote.

Katibu Mkuu James amesema kuwa kuzingatia kwa fedha zitumikazo katika utekelezwaji wa miradi ya Serikali kwa kiasi kikubwa hutumika kupitia mifumo ya ununuzi wa umma na kwamba jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuliimarisha eneo hilo ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika kupitia  ununuzi wa bidhaa.

Amesema taasisi za  umma  ambazo tayari  zimeunganishwa  katika mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki ni jumla ya taasisi nunuzi 418 kati ya taasisi 540 sawa na asilimia 77.4 ya taasisi nunuzi zilizopo nchini zimeunganishwa na mfumo huo.

James amesema tangu kuanza kwa mfumo huo kumeongeza ushindani kwenye michakato  ya ununuzi ,kuongeza ufanisi na hivyo kupunguza muda unaotumika katika michakato ya zabuni  pamoja kuongeza uwazi hivyo kupunguza vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Mhandisi  Leonard Kapongo amesema baada ya kupewa maagizo na Serikali waliingia kazini kuongeza katika kutoa mafunzo kuhusiana na mfumo kwa maafisa  Ununuzi na Tehama wa Taasisi za Umma.

Amesema hawataruhusu taasisi za umma kufanya nunuzi nje ya mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki kufikia Januari 31 mwaka ujao.

Mhandisi Kapongo amesema taasisi ambazo hazjaunganishwa wajiunge ikiwa ni pamoja na kugharamia mafunzo maakumu ya namna ya kutumia mfumo wa ununuzi kwa njia ya kieletroniki.

 Pichani kati ni Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dar,kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS)  ikiwa pamoja na Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri wa Fedha kuhusu matumizi ya mfumo huo.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Bodi  wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Balozi Dkt Matern Lumbanga na kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA),Mhandisi Leonard Kapongo.
 Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali-Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiwaonesha Waandishi wa Habari moja ya Nyaraka iliyokuwa na maelekezo ya uanzishwaji mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (TANePS),ambapo amesema Serikali imeagiza Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) ifikapo Disembe 31,2019 ihakikishe taasisi zote za ununuzi hapa nchini ziwe zimeungwa katika mfumo huo na kuanza kuutumia bila kisingizio chochote. Picha na Michuzi JR.(MMG).
 Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33EdhUD
via

Post a Comment

0 Comments