Ticker

10/recent/ticker-posts

Serikali yaipongea Taasisi ya CCBRT kutoa huduma kwa jamii kwa miaka 25

Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.

Akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa, Rais wa bodi ya CCBRT Tanzania, Dkt. Wilbrod Slaa alisema tulianzisha hospitali ya CCBRT mwaka 1994 mwezi wa Nne tukiwa na malengo ya kusaidia watoto wenye ulemavu, lakini wazo lilikuja nikiwa na Dan Wood tukiwa Zanzibar baada ya ajali ya ndege iliyotokea Rwanda 

" Nakumbuka mwanzo tulikuwa tunapita mitaani kwenye nyumba na kukuta watoto wenye matatizo ya miguu na macho, kuna nyumba tulikuta mtoto ambaye alikuwa hana uwezo wa kuona mchana lakini usiku anaona vizuri wataalamu wanakumbuka , huyu ndio alikuwa mgonjwa wetu wa kwanza". alisema Slaa. Kina mama wengi ilikuwa tukipita mitaani walikuwa wanalia kuomba msaada wa watoto wao wenye matatizo mbalimbali na tuliweza kuwasiadia 

Tulipata changamoto ya kupata sehemu ya kufanyia operesheni, ikabidi tuende hospitali ya Mwananyamala na kuomba kupewa ruhusa ya kuwafanyia operesheni wagonjwa wetu wakaturuhusu na changamoto nyingine ilikuwa mahali pa kulaza wagonjwa wetu, na ilibidi tukiuke taratibu na kwenda kuwapangishia kwenye nyumba ya kulala wageni ambazo tulikodi kwa wagonjwa tu, na kwa bahati waziri wa afya kipindi hicho, mhe. Anna Abdallah alitoa baraka zake wagonjwa waweze kuwekwa kwenye nyumba hiyo. Aliendelea kusema Dkt. Slaa

Tunashukuru serikali ya Tanzania kuwa mdau mkubwa sana wa CCBRT kwa kutoa ardhi kubwa bure  kuwezesha kujenga hospitali na kupandisha hadhi hospitali yetu kuwa ya rufaa (zonal referral) alisema Dkt. Slaa

Pia tunatoa huduma zetu kulingana na wagonjwa tunaowapokea, hii inategemea mgongwa private au sio private na gharama tunazowachaji wagonjwa wa private zinaenda kutibia wagongwa wasio na uwezo gharama za matibabu alimaliza kusema Dkt. Slaa

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alisema, Naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Taasisi ya CCBRT kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini. Najua mmepitia changamoto nyingi sana pindi mlipoanza kama alivyokwisha kusema Rais wa bodi ya Taasisi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa.

Pia niwapongeze kwa kuwa na huduma za mkoba (mobile outreach) ambazo zimekuwa na ubia na hospitali mbalimbali nchini kama vile Bombo mkoani Tanga, Seko Toure Mwanza, Mnazi Mmoja Zanzibar, Kabanga Kigoma, Bagamoyo na Ikwiriri hii inaonyesha jinsi gani mmeweza kuwa bega kwa bega nasi serikali alisema Mhe. Mwalimu.
Nachukua fursa hii pia kuwapongeza, kituo cha CCBRT Moshi ambacho kinafanya kazi nzuri sana, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 kimeweza kuhudumia watoto wenye ulemavu na familia zao zaidi ya 10,000 na kuwarejeshea matumaini aliendelea Mhe. Mwalimu

Nimepewa taarifa CCBRT ndani ya miaka 9 mnashirikiana na timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya mkoa wa Dar es salaam kutoa mafunzo kwa watoa huduma zaidi ya 900 kila mwaka hasa kwa madaktari na wauguzi. Na mradi wa kuwajengea uwezo watumishi kwenye vituo vya afya na zahanati 22 katika manispaa zote tano za mkoa wa Dar es salaam na Pia mradi huu umewekeza kiasi kikubwa cha miundombinu, ukarabati wa wodi za wazazi, ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,895,615,400 na uwekezaji wa vyumba maalum vya watoto njiti, vyoo maalum kwa wenye ulemavu, utambuzi wa mapema wa watoto wenye ulemavu na kina mama wenye fistula ya uzazi aliendelea kusema Mwalimu.

Kwenye fistula wastani ya akina mama 800 kwa mwaka walipata huduma ya upasuaji, takwimu zinaonyesha akima mama takribani 2000 hadi 3000 hupata fistula ya uzazi nchini , CCBRT kushirikiana na MUHAS, Chuo kikuu Dodoma, KCMC kumewezesha kutoa mafunzo na Taasisi ya kimataifa ya madaktari bingwa magonjwa ya kinamama na wajawazito,(figo) kuwa miongoni mwa vituo vya mafunzo ya upasuaji fistula duniani, na mpaka kufikia mwezi 10 mwaka 2019 watakuwa wamefanya upasuaji fistula kina mama wapatao 10,000 alimaliza kusema.

Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 4.5 huku Dkt. Wilbrod Slaa akimpongeza mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya  hospitali ya CCBRT jana jijini Dar es Salaam 
 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi akizungumza na wageni waalikwa
 Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa PWC kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 2 ili kuchangia gharama za matibabu kwa wasiojiweza

 Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya  CCBRT, Wilbrod Slaa akibadilishana mawazo na  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya  CCBRT, Wilbrod Slaa (kulia) akimkabidhi picha ya zawadi kwa mchango alioutoa kwa taasisi hiyo Makamu wa zamani wa Rais bodi ya CCBRT, Biharilal Tanna , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 
 Baadhi ya wakina mama waliopokea vyeti vya kutambua mchango wao kwa CCBRT wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangina Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi

 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija ya CCBRT usiku wa jana

 Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya CCBRT, Wilbrod Slaa (wapili kulia waliokaa) Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi na Makamu wa Rais wa zamani wa bodi hiyo, Biharilal Tanna na wadau mbalimbali kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi ya  hospitali ya CCBRT  jijini Dar es Salaam jana.

Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na  wafanyakazi wa Taasisi ya hospitali ya CCBRT jana kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rwRNLe
via

Post a Comment

0 Comments