SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTAFUTA SULUHU YA SUMU KUVU

  Masama Blog      
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na wadau wa mkutano unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumukuvu ,wanaotoka katika Nchi 15 za Afrika katika mkutano unaofanyika katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha leo.
Washiriki wa Mkutano unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumu kuvu wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Kilimo Mhe.Josephat Hasunga.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewataka Wakulima kuchukua hatua kudhibiti sumukuvu ambayo imekua ikiathiri mazao tangu yanapokua shambani na baada ya kuvunwa ili kuondokana na sumu hiyo yenye madhara inayosababisha saratani na hata kupelekea vifo.

Akizungumza katika mkutano wa wadau hao Mhe.Hasunga amesema kuwa serikali imeanza kushirikiana na wadau katika kutafuta suluhulu ya wakulima kuyakinga mazao yao na sumu kuvu na tayari wamekuja na dawa itakayowasaidia kudhibiti sumu hiyo kabla na baada ya mazao kuvunwa.

Amesema mkutano huo unaojadili juu ya Namna ya kudhibiti Sumu kuvu , lengo lake ni kukaa na kujadiliana kwa kina na kuona ni hatua gani zichukuliwe ,ili kuhakikisha kwamba wanapambana na ugonjwa huo sambamba na kutoa hamasa na elimu kwa wakulima,juu ya ugonjwa huo wa sumukuvu.

Hasunga amesema tayari Serikali imekuja na mkakati uliozinduliwa kipindi mkoani Simiyu kipindi cha sikukuu ya nanenane na umeshaanza kutekelezwa katika programu inayotambulika kama TANIPAC ,ambapo moja ya mambo yanayotekelezwa katika mradi huo ni kuhakikisha kuwa wanajenga magala,kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuepukana na sumu Kuvu 

Aidha amesema Utafiti uliofanywa na wataalamu wa nchi mbalimbali unaonyesha kwamba takribani asilimia 20%-40% ya mazao mbalimbali ya nafaka yamnaathiriwa na ugonjwa wa sumu kuvu.

Waziri amewataka Watafiti kufanya utafiti juu ya sumu kuvu na kuangalia hali halisi ya tatizo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa watafiti itakayosaidia kuchukua hatua zaidi.

Mratibu wa Utekelezaji Mradi wa Kudhibiti Sumu kuvu nchini,Clepin Josephat ,Mtaalamu amesema kuwa mwaka 2016 baadhi ya watu walifariki kutokana na sumu kuvu ,ambayo haionekani na haishikiki hivyo serikali ipo kwenye mpango wa kujenga maabara kubwa ya kilimo itakayosaidia kukabiliana na tatizo hilo.

Mtafiti Mwandamizi wa Teknolojia ya kudhibiti sumu kuvu ya Aflasafe kutoka shirika la IITA Ranajit Bandyopadhyay ,amesema kuwa baada ya utafiti wao na kupata dawa ya kudhibiti sumu kuvu wamekuja na mikakati ya kusambaza taifiti hiyo na dawa ili iweze kusaidia wakulima baada ya kukaa katika maktaba .

Kwa mujihu wa takwimu za mwaka 2017 za Shirika la chakula na Kilimo Duniani,(FAO)Tanzania ininazalisha tani milioni 6 za mahindi,ipia inazalisha zaidi ya tani milioni 1 za karanga .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NgjKPT
via
logoblog

Thanks for reading SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUTAFUTA SULUHU YA SUMU KUVU

Previous
« Prev Post