Ticker

10/recent/ticker-posts

SERIKALI KUTOA MILIONI 13 KUKARABATI SEKONDARI YA MISUNGWI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa shilingi milioni 31 kwa shule ya Sekondari Misungwi ili kukamisha ujenzi wa bweni la wasichana.

Waziri Ndalichako ametoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alioofika shuleni hapo kukagua miundombinu ya shule hiyo ambapo amesema amefurahishwa kuona uongozi wa shule jiyo  umekuwa ukitumia fedha visiting na kuweka akiba ya fedha kidogokidogo ambazo zimewawezesha kuanza ujenzi wa bweni hilo

"Nimefurahishwa  na mpango wa shule wa kuhifadhi fedha kidogo kidogo mpaka wamepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike jitihada hizi ni kazima ziungwe mkono nami nikiwa waziri wa elimu natoa mchango wangu wa kuhakikisha naleta fedha za kumalizia " Amesema Waziri ndalichako.

Profesa Ndalichako amesema pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi pia atahakikisha samani za bweni zinanuliwa  ili bweni hilo likamilike na kutumika.Aidha, Waziri Ndalichako amewata wanafunxi wa kike katika shule hiyo kuzingatia masomo yao wawapo shikeni hapo na kutojiingiza katika mambo ambayo yatawakatisha masomo yao na mwisho kupoteza ndoto zao.

Mkuu wa Shule ya sekondari Misungwi Mwanani Asembandwa amemshukuru Waziri wa Elimu kwa kutambua jitihada za shule za kuweka fedha kidogokidogo kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana 

Asembandwa amesema shule hiyo imefanikiwa kuwekeza fedha kidogo kidogo mpaka ikafanikiwa kupata  miliini 44  ambazo zimetumiwa kuanza ujenzi wa bweni la wasichana ambalo likikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa wakati mmoja.

"Kukamilika kwa bweni hili kutasaidia kutatua changamoto ya sehemu ya kulala kwa wanafunzi wa kike wa shule  pamoja na kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa watoto wa kike wengi zaidi" Amesema Mkuu huyo wa Shule.

Naye Mwanafunzi wa shule hiyo Zemda Robert amemshukuru Waziri kwa kutoa ahadi hiyo ambayo inakwenda kupunguza changamoto ya malizi shukeni hapo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua eneo linalojengwa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Misungwi
 Moja ya jengo la bweni la wasichana katika shule ya sekondari Misungwi lililojengwa na serikali kupitia mradi wa EP4R.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Misungwi alipofika shuleni hapo kukagua mindombinu ya shule hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2K7GQpZ
via

Post a Comment

0 Comments