Ticker

10/recent/ticker-posts

Rushwa ya ngono inaondoa utu wa mwanamke-wadau


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

 WADAU wa kutetea ukatili wa kijinsia wamesema kuwa rushwa ya ngono  kwa wanawake waliofanyiwa lazima wapaze sauti zao ili kukomesha tabia hiyo katika kujenga utu kwa mwanamke.

Wakizungumza katika kongamano  la maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia wamesema kuwa wanawake wanaofanyiwa ukatili wa rushwa ya ngono wamekuwa wakibaki na maumivu huku wengine wakiendelea kuumizwa na rushwa hiyo.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao ni Chama cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA) , Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake , Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru)pamoja na Jeshi  la Polisi.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake Mary Rusimbe amesema rushwa ya ngono inarudisha nyuma maendeleo ya wanawake kutokana na baadhi ya wanaume kuhitaji rushwa ya ngono ili kuwawezesha.

Amesema wameanzisha mtandao wa pamoja wa kupaza sauti za  kupinga rushwa za ngono katika jamii ikiwa ni Wanawake kuzungumza mara anapoona ili kufanikisha jambo lake lazima atoe rushwa hiyo basi atoe taarifa katika vyombo husika kwa ajili ya kukomesha.

Amesema kuwa rushwa iko katika hata shule za msingi ,Sekondari ambapo hao wanafanyiwa na kisha wanakaa kimya hali ambayo inawafanya kubaki na majeraha.Rusimbe amesema kuwa kujenga tabia ya jamii kuacha kufumbia macho suala la rushwa ya ngono.

 Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 ya  kupinga ukatili wa kijinsia ni Kataa Rushwa ya Ngono ,Jenga Kizazi chenye usawa.

Mkurugenzi huyo amesema baadhi yao wanatumia madaraka vibaya sehemu mbalimbali kwa wanawake na wanaume kuwapandisha vyeo watu kwa ajili ya rushwa hali ambayo inaondoa utu wa kupanda kwa vyeo hivyo.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Canada Pamela O' Donnell amesema kuwa rushwa ya ngono ipo duniani kote hivyo mapambano hayo ni ya dunia nzima katika kupaza sauti.

Nae Mwakilishi wa Shirika wa Kimataifa linaloshughukia wanawake  Agnes Hanti amesema kuwa mapambano yaendelee katika kujenga utu wa watu katika kuondokana na rushwa  ya ngono.Mwnyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Rehema Ludanga amesema kuwa kwa wafanyakazi wanaofanyiwa kutoa taarifa na hatua zikachukuliwa.
 Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Christina Onyango  akizungumza kuhusiana namna jeshi la polisi linavyokabiliana na rushwa ya ngono
 Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa linaloshughukia wanawake Agnes Hanti akitoa namna Shirika hilo linavyoshirikiana n wadau katika kupinga ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono wakifatilia mada katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2L0kneR
via

Post a Comment

0 Comments