ROSE MANUMBA AINGIA ORODHA YA WAJUMBE WA KUSHAURI TAASISI YA UMOJA WA MATAIFA WANAWAKE TANZANIA (UN WOMEN TANZANIA).

  Masama Blog      
Msichana Rose Manumba Chini ya Umri wa Miaka 30,  ameingia Katika Orodha ya Wajumbe wa kushauri Taasisi ya Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (UN Women Tanzania) 2019 - 2021 

 Rose Manumba ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania, amechaguliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wanaotokana na Asasi za Kiraia kuingia katika kikundi cha kushauri (Civil Society Advisory Group) Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (UN Women Tanzania) namna gani tunaweza kufikia moja ya malengo ya maendeleo endelevu hususani lengo la 5 la Usawa wa Kijinsia (Gender Equality) katika maeneo mbalimbali.

Kikundi hicho cha washauri kina jumla ya Idadi ya Wajumbe wasiozidi 10 wanaotokea kwenye Taasisi mbalimbali.

Kikao cha kwanza kimefanyika  jana  Novemba 20/2019  na kufunguliwa rasmi na Naibu Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Wanawake Tanzania (Deputy Country Representative to UN Women Tanzania) Bi. Julie Taylor.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2O6Pvez
via
logoblog

Thanks for reading ROSE MANUMBA AINGIA ORODHA YA WAJUMBE WA KUSHAURI TAASISI YA UMOJA WA MATAIFA WANAWAKE TANZANIA (UN WOMEN TANZANIA).

Previous
« Prev Post