RC SONGWE ATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII ILEJE,AFURAHISHWA NA MRADI WA SHAMBA LA IYONDO-MSWIMA.

  Masama Blog      


RC wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela aliye mbele na DC wa Ileje Ndg.Joseph Mkude wakiwa kwenye Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange Wilayani Ileje
Mkuu wa Mkoa wa Songwe akiongozana na DC wa Ileje kutembelea kitalu cha miti cha Shamba la Iyondo Mswima.
Barabara ya Isoko hadi Katengele na Sange ikikatisha katikati ya msitu wa asili wa Iyondo Mswima wanamoishi nyani jamii ya mbega wenye rangi nyeupe na nyeusi moja ya vivutio vya utalii.
Mzee Yangison Mtawa aliye kushoto akitoa maelezo kwa RC Mwangela wa Songwe ambapo alielezea ugumu wa soko kwa bidhaa za mianzi anazozalisha.
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe na Wilaya ya Ileje wakigongeana glasi kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Mkuu wa Mkoa wao Nicodemas Mwangela aliyetimiza miaka 62.Na Daniel Mwambene Ileje Utalii

RC wa Songwe atembelea vivutio vya utalii wilayani Ileje afurahishwa na Mradi wa Shamba la Iyondo-Mswima akihimiza kulindwa kwa misitu ya asili iliyopo wilayani humo asherehekea siku yake ya kuzaliwa katika vilele vya milima ya shamba hilo.

Ukiwa ni mwisho wa juma siku ya Jumamosi Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemas Mwangela alitembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Ileje ikiwa ni sehemu ya utalii wa ndani kwa timu nzima aliyokuwa amefuatana nayo.

Ziara hiyo ya siku moja ilimwezesha kufika hadi Kijiji cha Ndembo mahali panapozalishwa nyungo zitokanazo na mianzi ambapo aliweza kukutana na wasukaji akiwahimiza kuungana kkatika vikundi ili kuweza kutambuliwa na serikali na kuongeza uzalishaji wenye tija.

Kiongozi huyo,aliweza kufika nyumbani kwa Mzee Mtawa akiagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanamsaidia kutafuta soko la bidhaa anazozalisha mzee huyo baada ya kuambiwa kuwa amekuwa akisubiri tu matukio kama vile nane nane na kimondo baada ya hapo bidhaa alizozalisha kwa gharama zikihifadhiwa.

Safari hiyo ikiendelea kwa kuupanda mlima Kashima ambao kwa madereva wengine huwa ni kipimo tosha cha fani hiyo kutokana na kona kali zilizofunikwa na misitu ya asili inayoongeza radhaa a utalii.

Alipofika katika Mradi wa Shamba la Miti wa Iyondo Mswima aliweza kupokea taarifa ya mradi huo toka kwa Meneja wa hamaba Ndg.Deograsian Kavishe akiridhishwa na taarifa hiyo jinsi inavyoakisi uhalisia wa mazingira ya eneo hilo na kuwa kiutio tosha cha kitalii.

Msafara ulielekea shamani ilikopandwa miti,huku macho yakiendelea kufaidi mandhari nzuri ya vilele vya milima vilivyofunikwa nyasi fupi ambazo baadeya zaweza potea kutokana na kufunikwa na miti inayoendelea kupandwa.

Mara baada ya kufika sehemu maalum iliyokuwa imeandaliwa likafanyika tukio la kukumbuka tarehe ya kuzaliwa kiongozi huyo yaani ikifurahiwa na kila mmoja kutokana na mahali ilipoandaliwa huku ikinyunyiziwa na manyunyu yaliyoshuka polepole yakiashiria neema na utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Mwisho wa safari yake ilikuwa ni katika Maporomoko ya Lusalala yaliyopo kwenye Mto Sange ambapo kuliweza kuwatoa jasho watalii hao wa ndani kutokana na mteremko mkali ambao haukuonesha kumteteresha Brigedia Jenerali huyo mstaafu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NYbVyo
via
logoblog

Thanks for reading RC SONGWE ATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII ILEJE,AFURAHISHWA NA MRADI WA SHAMBA LA IYONDO-MSWIMA.

Previous
« Prev Post