RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA YAKE DODOMA KESHO

  Masama Blog      
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake wakati akitoa taarifa kuhusiana na ziara ya kikazi ya Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,itakayoanza kesho tarehe 21 hadi Novemba 25,mwaka huu jijini Dodoma,upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobasi Katambi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka.

Rais Dk John Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Dodoma Novemba 21,2019 ambapo katika ziara hiyo ataweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya mandeleo ikiwemo Hospitali ya Uhuru, Stendi Kuu ya mabasi pamoja na soko kuu Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amesema ziara hiyo itaanza Novemba 21 mwaka huu ambapo Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya kumi (10) ya Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga, Chuoni hapo.

Dk Mahenge amesema Novemba 22, 2019 Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Hospitali ya Uhuru, Wilayani Chamwino, ujenzi wa nyumba 118 za Askari Polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medeli East, Ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi iliyopo Nzuguni.

Miradi mingine ni Soko Kuu linalojengwa katika eneo la Nzuguni  pamoja kuzungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika stendi ya mabasi Nzuguni.

“Jumatatu Novemba 25, 2019 mheshimiwa Rais ataweka mawe ya msingi kwenye miradi ya ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Kikombo, ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji na Ujenzi wa jengo la Makandarasi katika eneo la National Capital City.

Ziara hii ya mheshimiwa  Rais (John Magufuli) kwetu ni fursa ya kumwonesha hatua tulizofikia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyotupatia na kupokea maelekezo ya namna ya kusonga mbele kwa uhakika katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake,” Amesema Dk Maheng


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2O0QKMe
via
logoblog

Thanks for reading RAIS MAGUFULI KUANZA ZIARA YAKE DODOMA KESHO

Previous
« Prev Post