RAIS DKT. MAGUFULI AIMWAGIA SIFA DAWASA KWA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI

  Masama Blog      
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (katikati) akipokea gawio lenye thamani ya Bilioni 1.3 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili kulia)  akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akishudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto). Picha zote na Othman Michuzi, Dodoma.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli ameipongeza Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kuweza kuwasilisha gawio la Bilioni 1.3

Dkt Magufuli amepokea jumla ya Trilioni 1.05 kutoka taasisi, mashirika na makampuni, hafla iliyofanyika leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

Hayo ameyasema leo wakati wa hafla ya kupokea kwa michango, gawio na  ziada kutoka kwa Tasisis, mashirika na makampuni yenye umiliki wa serikali au hisa.

Akitoa pongezi hizo, Magufuli amesema yapo mashirika na taasisi mbalimbali hazijapelekea gawio ila anampongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Dawasa Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange kwa kufanikisha mamlaka hiyo kutoa gawio.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja, katika hafla ya kukabidhi Gawio kwa Serikali, iliyofanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma leo. 

"Jenerali Mwamunyange emeleta gawio, ametoka katika ukuu wa majeshi nimempeleka katika maji (Dawasa) na amefanya vizuri , hongera sana", amesema Magufuli.

Amesema, kutokana na hilo anaamini kuwa wenyeviti wa bodi wakiwa Wanajeshi basi mashirika yataenda vizuri katika uendeshaji na kila mwaka gawio litakuwa kinazidi.

"Kuna jumla ya mashirika, taasisi na makampuni karibu 266 lakini ukiangalia walioleta ni 79, yapo mengine 187 hayajaleta nakuagiza Waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango awatumie barua nawapa siku 60 walete gawio au wakishindwa tuyataifishe," amesema.
Aidha, amesema ndani ya miaka mitano kuanzia 2014-15 mashirikia yaliyotoa gawio yalikuwa ni 24 walikabidhi jumla ya Bilioni 130, kwa mwaka 2015-16 yalikuwa ni 25 yakikabidhi bilion 249, mwaka 2016-17 yakipanda hadi 38  wakitoa gawio la bilioni 677 na kwa mwaka 2017-18 yakiwa 40 wakikabidhi bilioni 842. Pia kwa mwaka wa 2018-19 mashirika na taasisi zilipanda hadi kufikia 79 wakitoa jumla ya Trilioni  1.05.

Dawasa wamekuwa moja kati ya taasisi na mashirika ya Serikali 79 yaliyotoa gawio la Bilion 1.3 kwa serikali.

Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa mamlaka kutoa gawio kwa serikali na kwa mwaka huu wamekabidhi bilioni 1.3 kwa mwaka 2018-19.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37yFTB2
via
logoblog

Thanks for reading RAIS DKT. MAGUFULI AIMWAGIA SIFA DAWASA KWA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI

Previous
« Prev Post