Ticker

10/recent/ticker-posts

RAIS DK.MAGUFULI APOKEA GAWIO LA SH.BILIONI 11 KWA MWAKA 2018 KUTOKA PUMA ENERGY TANZANIA

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imetangaza gawio la Sh.bilioni 22 kwa wanahisa wake kwa mwaka 2019 ambapo leo Novemba 24 imekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Dk.John Magufuli Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Taarifa ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari imefafanua kwa kina kuwa kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. 

Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.

Imeelezwa kuwa majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta 94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.

Taarifa hiyo imesema kufikia mwisho wa mwaka ulioishia Desemba 31 2018 kampuni ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla ya Shilingi bilioni 25. Kampuni iliwekeza takribani shilingi bilioni 16 kwa mwaka 2018 kununua na kuendeleza miundombinu ikiwemo ukamilishwaji wa mfumo wa kujazia mafuta katika jengo namba Tatu (Termina 3) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar e salaam.

Pia ununuzi wa vituo viwili vya mafuta kwenye jiji la Dodoma ikiwa ni kuiunga serekali mkono katika kuhamia Dodoma.

"Wakurugenzi wa kampuni wamependekeza gawio la Sh.bilioni 22 bolioni kwa mwaka ulioishia Disemba 2018. Hivyo Kila mwanahisa atapata shilingi 11 bilioni. (2017 gawio lilikuwa 18 bilioni, 2016 gawio lilikua 14 bilioni na 2015 gawio lilikua 9 bilioni.) 

"Kutokana na utendaji mzuri wa kampuni ya Puma Energy, gawio limekua kwa asilimia 57 ikilinganishwa na gawio la mwaka 2016 na kwa asilimia 22 ikilinganishwa na gawio na mwaka 2017. 

"Ukuaji huu unaendana sambamba na mikakati ya kampuni ya kuhakiksha kampuni inaendelea kukua, kutengeneza faida, kukuza ajira nchini, kuchangia pato la taifa kupitia kodi, na kuendelea kuiunga serekali mkono katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo,"imesema taarifa hiyo

Dominic Dhanah, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Limited amesema kuwa ufanisi wa kibiashara wa Puma Energy Tanzania kwa mwaka 2018 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzo pamoja na mapato. Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndio tunaongoza katika soko. 

Pia ameongeza kuwa taaarifa za masoko zilizochapishwa na Mamlaka ya udhibiti (EWURA) inaonesha kuwa uwepo wa Puma Energy kwenye soko la mafuta umeongezeka kutoka asilimia 12% mwaka 2015 hadi asilimia 14 kwa mwaka 2017

Dhanah pia amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake katika mikakati yake ya kukusanya kodi, kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani na kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyooneshwa kwenye bajeti ya 2019/20. 

Amesema kuwa mikakati hiyo imewezesha PumaEnergy Tanzania kupata kazi ya kuuza mafuta katika mradi wa reli ya kati “standa gauge”, mradi wa bwawa la umeme la Mwl. Nyerere kule Rufiji, Daraja jipya la Salender na miradi mingine mingi ya kimkakati.

" Miradi hii mikubwa inatoa fursa kwa wawekezaji mbali mbali kufanya biashara na kufanya makampuni mengi ikiwemo Puma kutengeneza faida zaidi. Puma itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Awamu ya tano, na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya taifa, hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa hundi ya gawio yenye thamani ya Bilioni 11 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA Energy Tanzania Dkt Selemani Majige (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Ofisa Mawasiliano na Mwanasheria wa Kampuni hiyo Goodluck Shirima (kulia). Gawio hilo limekabidhiwa leo Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Selemani Majige(wa kwanza kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa wakati wa tukio la kampuni,mashirika na Taasisi zikabidhi gawio kwa Serikali ambapo Rais Magufuli amepokea gawio leo Novemba 24,2019 Ikulu Chamwino jijini Dodoma
Godluck Shirima kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania(wa kwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa ghafla ya Taasisi, Mashirika na Kampuni kukabidhi gawio kwa Serikali,ambapo Kampuni ya Puma amekabidhi gawio la Sh.bilioni 11 kwa Rais Magufuli leo Novemba 24,Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma
 Rais Dk.John Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi,Mashirika na Kampuni baada ya tukio la kukabidhiwa kwa gawio iliyofanyika leo Novemba 24 Ikulu Mjini Dodoma


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qIvORj
via

Post a Comment

0 Comments