RADI YAUWA MMOJA ARUMERU NA KUJERUHI WATANO

  Masama Blog      
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Mtoto mmoja aliejulikana kwa jina la Mejoole Melau Loitale (14) amefariki dunia na wengine wa tano kujeruliwa mara baada ya Radi kubwa ilioambatana na mvua kubwa ilionyesha katika kata ya Sambaya wilayani Arumeru.

Akiongelea tukio hilo mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa tukio hilo lilitokea November 23 majira ya jioni ambapo zilitokea mvua kubwa ambazo ziliambatana na Radi ilipiga na kusababisha madhara ya watu sita, akiwemo mtoto ambaye alifariki wakati wa jitihada za kumkimbiza hospital zikifanyika .

Aidha alibainisha kuwa majeruhi mmoja amelazwa katika hospitali ya Seliani Ngaramtoni ambae ametambuliwa kwa jina la Melau likindasaru loita ( 35 )anaendelea vizuri huku majeruhi wengine wanne wameruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutopata madhara makubwa.

Muro alitoa Rai kwa wananchi wote wa Arumeru kuendelea kuchukua tahadhari wakati wa kipindi hiki cha mvua kikiendelea kwa kuhakikisha hawakai chini ya miti, au kwenye nguzo za nyaya za umeme.

Alitumia muda huo kutoa pole na rambirambi kwa familia ya Marehemu na kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurejea katika shughuli zao za kawaida za kijamii. 

Aliongeza kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama , kwa kushirikiana na vikosi vya zimamoto na uokoaji viko katika hali ya tahadhari na utayari mkubwa wa kukabiliana na majanga yeyote yatakayo weza kutokea hivyo aliwataka wananchi kukaa na amani kwani Serikali ipo kwa ajili yao .from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KOe9yB
via
logoblog

Thanks for reading RADI YAUWA MMOJA ARUMERU NA KUJERUHI WATANO

Previous
« Prev Post