Ticker

10/recent/ticker-posts

Mwenyekiti wa Tahliso afanya Kikao Kazi na Balozi wa Tanzania Nchini China

Mwenyekiti wa Tahliso Ndg.Peter Niboye akiwa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania Nchini China Mh.Balozi Mbelwa Kairuki

Beijing China

Mwenyekiti wa Tahliso Ndg.Peter Niboye amefanya leo kikao cha kazi na Balozi wa Tanzania Nchini China Mh.Balozi Mbelwa Kairuki na kujadiliana kwa pamoja jinsi ya Kuhakikisha Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu Nchini Tanzania na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China wanaweza wakanufaikaje na Fursa zilizopo Nchi ya China na Kuzileta Tanzania na hii yote ni kuhakikisha Vijana wa Tanzania tunaisaidia Serikali ya Awamu ya Tano Kutekeleza kwa pamoja Sera ya Viwanda kwa Vitendo.

Lakini Pia kwenye Kikao hicho Balozi ameahidi Ushirikiano wa Kutosha kwa Tahliso na kuahidi kuendelea kuhakikisha Fursa za Scholarships kuendelea kupatikana na kama Tahliso tuendelee kusaidia kuzitangaza Fursa hizi ili Watanzania wengi wapate fursa ya kusoma lakini Pia Balozi ameahidi kuendelea kushirikiana na Jumuiya za Wanafanzi kwani ndo think tankers wa Taifa letu na kuhakikisha Fursa za Viwanda zitakazopatikana tuzitumie vizuri kwa manufaa mapana ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Tahliso aliwasilisha salamu kutoka Tanzania pamoja na Tahliso kwa ujumla na kuomba kuendeleza Ushirikiano baina ya Tahliso na Ubalozi wa Tanzania Nchini China na kuahidi Ushirikiano ulioanza utadumu na lazima Vijana sasa tuanze kufanya Kazi kwa Bidii na kutafuta fursa zilizopo kwa wenzetu ili kuhakikisha tunazileta Nyumbani na kuzitekeleza kwa Wakati.

Lakini pia tumekubaliana Kuhakikisha Changamoto zote za Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma China wanazokumbana nazo tutazishughulikia kwa Pamoja ili kuhakikisha wanapata mazingira mazuri ya Kusoma wawapo Nchini China.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma Beijing China pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania Nchini China.

Tanzania na China ni Marafiki wakubwa na sisi kama Vijana wa Taifa letu tunakila Sababu ya Kuhakikisha tunatumia fursa zilizopo kwa Kufanya kazi kwa Bidii.






from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36nJz8d
via

Post a Comment

0 Comments