Ticker

10/recent/ticker-posts

MWENYEKITI CABCT AWAASA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania (CABCT) akitoa cheti kwa mmoja ya wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba katika Shule ya Msingi Magoro iliyopo wilayani Rufiji.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania (CABCT) Xian Ding akizungumza wakati wa mahafali ya 55 ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mahoro iliyopo Rufiji mkoani Pwani.Ding alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania 
(CABCT)Xian Ding amesema ipo haja kwa wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi  vyuo vikuu nchini kusoma kwa bidii ili kufikia maendeleo endelevu ya kiuchumi  huku wakilenga kuanzisha biashara kubwa, kuajiriwa au kubuni teknolojia za kisasa katika kuendeleza nchi. 

Ameyasema hayo katika mahafali ya 55 ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi Mohoro iliyopo Rufiji mkoani Pwani alipokuwa mgeni rasmi ambapo pia ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kufundishia katika shule hiyo.

 “Naipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya elimu kwenye shule 
hii na shule zingine, sisi wachina tutaendelea kusaidia kwenye jambo hili la 
elimu” alisema Bw. Ding.

Wakati anatoa hotuba yake Ding amewashauri wahitimu kuzingatia elimu na kuwaeleza bayana kuwa wazazi wamewekeza kwao. Aidha ameeleza ili uchumi uweze kukua mahali popote pale kunahitajika watu wabunifu waliobobea kwenye fani mbalimbali hatua inayotokana na kusoma kwa bidii na kujituma katika elimu. 

Pia Mwenyekiti huyo amewahamasiaha wahitimu mmoja mmoja kuzingatia elimu na kuwaambia kuwa hapo baadae utakapohitaji kuwa Daktari lazima usome, ukitaka kuwa Rubani lazima usome, ukitaka kuwa Waziri lazima usome, ukitaka kuwa Mbunge lazima usome, ukitaka kuwa Injinia lazima usome, ukitaka kuwa  Mwalimu lazima usome. 

“Nawaomba sana wanafunzi msome kwa bidii ili mje kujenga Taifa letu zuri la  Tanzania sambamba na kusimamia sera ya kukuza uchumi wa viwanda,” 
amesema Ding.

Ding ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Huatan Invesment Group 
inayomiliki miradi ya uwekezaji nchini ikiwamo kiwanda cha kutengeneza chakula  cha mifugo Pugu na kiwanda cha kuchakata betri zilizokwisha muda wake Rufiji.  

Katika kutekeleza Sera ya kushirikiana na jamii inayomzunguka, kwenye 
mahafali hayo, Mwenyekiti huyo ametoa msaada wa viatu kwa wanafunzi 
wanaobaki wa darasa la tatu na nne na fedha taslim kama zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika mitihani yao  ili kuwapa motisha wanafunzi wanaoendelea na masomo.

Katika hatua ya kusaidia maendeleo ya elimu Wilayani Rufiji, Mwenyenkiti huyo ametoa fedha kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamwage waliokaa kambini kujisomea. 

Hata hivyo imekuwa ni kawaida kwa Mwenyekiti huyo wa CABCT kuunga mkono masuala mbalimbali ya jamii yanayojitokeza katika maeneo wanayofanyia  biashara na uwekezaji wao ikiwamo (usafiri, afya na elimu).  Jambo hili ni zuri na linapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OawRkP
via

Post a Comment

0 Comments