Ticker

10/recent/ticker-posts

MTANZANIA ASHINDA TUZO YA LEGACY JIJINI LONDON

Kijana Mtanzania Erick Venant, amepokea tuzo ya Legacy jijini London,Tuzo hiyo imetolewa Novemba 26/2019, wa Kutambua mchango wake katika kupambana na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Antimicrobial resistance)na haswa kuongeza uelewa kwenye Jamii na kutia hamasa ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tatizo hili, juhudi zake zinatajwa kuwa muhimu katika kuboresha afya ya ulimwengu*.

Akiwa Uingereza Erick amepata nafasi ya kukutana na Prince William katika makazi ya Kifalme, Kengstone palace ambapo walijadili kwa ufupi kuhusu tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

 Magazeti ya Uingereza yameripoti jinsi Prince William alivyotumia lugha ya Kiswahili mara kadhaa wakati wa mazungumzo hayo.Erick ni miongoni mwa vijana 20 duniani waliochaguliwa kupokea tuzo ya Legacy waandaji wa tuzo hiyo "The Diana award" wanasema vijana wote waliochaguliwa wana mchango mkubwa kwenye jamii.

Washindi wengine wametoka mataifa ya Uingereza, Malaysia, India,Canada, Nigeria na Nepal.Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Elizabeth Nyamayaro na mtendaji mkuu wa Shirika la ndege la Uingereza Alex Cruz ni miongoni mwa waliounda jopo la majaji 14 waliokutana kuchagua washindi 20 wa tuzo hii kutoka miongoni mwa washindi wa tuzo ya Diana award wa mwaka 2018 na 2019.

Sherehe za Utoaji wa tuzo zilifanyika katika ukumbi wa Old Royal Naval College,Greenwich-London na kuhudhuriwa na kaka mkubwa wa Princess Diana, Earl Spencer.Tuzo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.Tuzo za Diana award na Legacy award hutolewa kama kumbukumbu ya Princess Diana wa Wales aliyefariki mwaka 1997.Watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo hilo.
 Kijana Erick Venant akiwa na tuzo yake  ya Legacy jijini London.
Kijana Mtanzania Erick Venant, akipongezwa na Prince William baada ya kukaribishwa kwenye makazi ya kifalme,Kingstone Palace kwa kupokea  tuzo ya Legacy jijini London.Tuzo hiyo imetolewa  Novemba 26,2019.
 Muonekano wa tuzo yenyewe.
 Picha ya pamoja na Wadau


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2rAIxpk
via

Post a Comment

0 Comments