MTANDAO WA UTAFITI WA KISAYANSI LAZIMA UANZIE KATIKA VYUO VIKUU

  Masama Blog      
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya utafiti ya taifa nchini Afrika Kusini, Dkt. Molapo Qhobela kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliojumuisha wanasayansi wa nchi 15 za kusini mwa jangwa la Sahara.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia , Amos Nungu.

Dkt. Qhobela amesema kuwa tafiti zitakazofanywa ziwe za afya, kilimo pamoja na chakula zote ziwe kwa kushirikiana ili kuleta matokeo mazuri kwa kujifunza kwa kila nchi ambayo hufanya utafiti kwa kubadilishana uzoefu katika utafiti.

Amesema ili utafiti ufanikiwe nilazima kuwe na ushirikiano na kubadilishana mawazo kati ya nchi zinazofanya utafiti za kisayansi.

Dkt. Qhobela nchi za kisayansi za Afrika zisifikiri kuwa hazina vitu vizuri vya kufanyia utafiti iwe katika Afya, Chakula, Kilimo na hata Mazingira.

"Sisi kama Jumuia Tunafanya kazi kwa karibu ili kuweka Sayansi iwe wazi  kwani Sayansi ya Afrika inategemea utafiti wa mwenzie". Amesema Dkt. Qhobela.
 Dkt. Merody Mentz, Coetzee akizungumza a waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Sayansi, Teknolojia na ubunifu. amesema kuwa lazima mtandao wa utafiti kuanzia kuboreshwa katika vyuo vikuu mbalimbali katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara ili kuweza kuwa na watafiti wengi ambao ni vijana.

Amesema changamoto kubwa ni kutokushirikia kwa watafiti endapo utafiti unafanywa. Ameshauri kuwa na ushirikiana kati ya watafiti wa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Mwakilishi shirika la Canada linalofadhili Utafiti katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Dkt.Ellie Osir akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Dkt. Osir amesema kuwa Suala la kisayansi liwekewe kipaumbele  na ameshauri iwe ajenda ya nchi za Afrika katika kufanya utafiti wa Kisayansi, Teknolojia na ubunifu.

Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu unaoendelea katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nungu amesema kuwa mijadala inayoendeshwa wabunifu kutoka katika Jangwa la Sahara wanachangia na mwisho wa siku kutakuwa na matokeo mazuri ya katika kubadilishana mawazo ya kiutafiti na ubunifu.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2O9lFVH
via
logoblog

Thanks for reading MTANDAO WA UTAFITI WA KISAYANSI LAZIMA UANZIE KATIKA VYUO VIKUU

Previous
« Prev Post