MLEMAVU WA MACHO ATAMANI KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA

  Masama Blog      
Na Woinde Shizza, Globu ya jamii Arusha
KIJANA Baraka Imanuel ni kijana mwenye umri wa miaka (24) mkazi wa ngaramtoni halmashauri Arusha iliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, kijana huyu ni mlemavu wa macho (kipofu ) na ni mfanyabiashara ndogomdogo na malengo yake ya kutoka kumiliki biashara ndogo anayoifanya na kuwa mfanyabiashara mkubwa.

Gazeti hili lilipata nafasi ya kuzungumza na kijana huyu na alikuwa na
mengi yakueleza kuhusiana na namna anavyofanya biashara yake

Baraka anafanya biashara ya kuuza viberiti ndani ya jiji la Arusha, kila
asubuhi amekuwa akiamka na kwenda kununua viberiti na kuvitembeza kwa watu mbalimbali na kuuza ili apate chochote kitu kitakacho msaidia kutumia yeye na familia yake.

Baraka ni mtoto wa kwanza katika familia ya mama Beatrice Imanuel
akiwa na wadogo zake wawili mmoja wa kike alimtaja kwa jina la Jackile
Imanuel ambaye yeye yupo nyumbani tu hafanyi kazi yoyote pamoja na
wakiume aliyemtaja kwa jina la Steven Imanuel ambaye yeye ni
anajitolea kufanya kazi ya kusaidia mafundi wa ujenzi ili apate
chochote kitu cha kuwasukuma katika maisha.

Anafafanua kuwa mama yake mzazi anafanya bishara ya mamantile huku
baba yake aliemzaa aliikimbia familia na kutelekeza na kukimbili
pasipo julikana kwa kipindi cha mda mrefu.

Kwanini alianza biashara ilihali ni mlemavu wa macho?
Anaeleza kuwa kitu halisi kilichomsukuma mpaka akaamua kufanya
biashara ya kutembeza viberiti ni kuondokana na utegemezi, kitu
ambacho alisema anakichukia kuliko vitu vyote katika maisha yake japo
kuwa yeye ni kipofu.

Alisema kuwa aliamua kumuomba mama yake mtaji wa kuanza biashara hali kuwa mama yake alikuwa mgumu wa kumpa kutokana na hali yake lakini alimbembeleza hadi mama yake akaamua kumpa mtaji wa shilingi elfu 30, hela ambayo aliamua kwenda kununua nusu katoni ya viberiti na kuanza
kutembeza.

“Mama alinipa mtaji wa shilingi elfu 3o tu na niliamua kuanza
biashara bila kujali hali yangu na mpaka leo nafanya, nilianza na nusu
katoni ya viberiti na sasa hivi naweza nunua katoni moja nzima mbali na
hivyo pia nashukuru Mungu mtaji wangu umekuwa na umefikia kiasi cha
shilingi elfu 70 na hii inatokana na mimi kujali kazi yangu na
kuipenda na pia kuafanya maamuzi ya kutokuwa tegemezi”alibainisha
Baraka.

Anatambuaje Fedha anapopewa na mteja ?
Baraka alifafanua kuwa alibahatika kusoma hadi kidato cha nne ambapo
alisema kuwa elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi Longido mkoani Arusha, huku elimu ya sekondari akiipata katika shule ya Shaibushe iliopo mkoani Shinyanga ambapo walikuwa wakifundishwa na walimu wenye uzoefu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye uhitaji.

“Nikipewa ela najua hii ni shilingi ngapi kutokana na elimu niliopewa
darasani pia nakisia na kutambua hii ni kiasi gani, pia nashukuru Mungu
maana wateja wengi nao wauzia viberiti wananionea huruma hivyo
hawawezi kunirusha kwani wanaona kabisa hali yangu ilivyo”,alisema

Alibainisha kuwa amekuwa anaamuka kila siku asubui na kwenda kununua
viberiti hivyo katika maduka ya Jumla na amekuwaanatembeza katika
maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha ikiwemo standi, masokoni na hata
katika maeneo ya majumbani kwa watu.

Nini ombi lake kwa serikali na wadau ?
Baraka ameiomba serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza katika
kumsaidia kumuongezea mtaji na ikiwezekana kumfungulia sehemu moja
ambayo atakuwa anafanya biashara yake kwa kutulia na kuaachana na
kutembeza barabarani anavyofanya hivyo anahatarisha maisha yake
kwani anaweza kupata ajali kugongwa na hata kuibiwa mtaji wake mdogo
ambao ameukusanya kwa ajili ya kumkimu kimaisha.

Kwa upande wa mama yake Beatrice Imanuel alisema kuwa mtoto wake
Baraka alizaliwa na ulemavu wa macho lakini anashukuru Mungu
amejikubali na anajitambua pia anaweza kujituma hata kufanya biashara
tofauti na walemavu wengine ambao wengi wao wanaombamba omba tu
barabarani na hawana mawazo wa kugundua mradi wowote au biashara
yeyote ambayo inaweza kuwasaidia katika maisha.

Anaongeza kuwa kijana wake amekuwa ni mtu wa kumsaidia katika baadhi
ya maitaji hapo nyumbani kwani amekuwa akinunua vitu mbalimbali na
hata mda mungine wadogo zake wakiumwa na yeye anafedha za kuwapeleka hospitali amekuwa akimega sehemu ya mtaji wake na kuutumia kwa jili ya kuwapeleka hospitali.

Beatrice ametoa wito kwa baadhi ya watu wenye ulemavu na kuwaambia
wasijizarahu pindi wanapokuwa walemavu bali wajaribu kuangali kitu cha
kufanya ambacho kitawakwamua kimaisha na kuachana na biashara ya kukaa na kuomba omba barabarani, pia aliwataka wazazi ambao wanawatoto ambao wanaulemavu wasiwafiche watoto wao ndani bali wawatoe nje wakapate elimu kama vile watoto wengine wanavyopata elimu kwani iwapo watapata elimu itawasaidia kujiongeza katika maisha.

“Nina imani mtoto wangu kama angekuwa hajapata elimu basi asingeweza
kuniomba hela ya mtaji na kujiamini na kwenda kuanzisha biashara
ya kuuza viberiti hii imetokana na kujiamini kwakwe na ndio maana
akaamua kujitoa na kwenda barabarani kufanya biashara naimani huu
wote ni ujasiri ambao alijengewa na walimu wake wakati alipokuwa
shuleni, na kwakweli ananisaidia sana katika maitaji madogo madogo
hapa nyumbani “Alisema Beatrice.

Baadhi ya wananchi ambao wanamshuhudia kijana
Baraka walimpongeza jinsi anavyofanya kazi na kusema kuwa ni vijana
wachache wenye ulemavu ambao wanaweza kujiongeza na kuanza kufanya
biashara kama vile kijana Baraka anavyofanya biashara, huku wengine
wakisikika wakisema ni bora angetafuta biashara ya kukaa sehemu moja
na kufanya na sio kutembeza kwa ajili ya usalama wa maisha yake.


Picha zikionyesha kijana Baraka Imanuel akiendelea kufanya biashara yake ya viberiti katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2C3le9O
via
logoblog

Thanks for reading MLEMAVU WA MACHO ATAMANI KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA

Previous
« Prev Post