Ticker

10/recent/ticker-posts

MIAKA KUMI YA KAKANGAGA SHULE YA BAKWATA INAYOPOKEA WAKIRISTO.


Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Shule ya Kiislamu ya KAKANGAGA MUSLIM SECONDARY SCHOOOL iliyopo Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, imetimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake, ikiwa tayari imekwisha hitimisha Vidato vya Nne mara nane toka Mwaka 2009.

Shule hiyo inayomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Kwa miaka mitano sasa imekuwa chini ya usimamizi madhubuti wa Uongozi wa Katoro Islamic Seminary, ambao pia ni wasimamizi wa Kahama Islamic, hali ambayo imechangia Mafanikio makubwa kwa Muda Mfupi toka ilipokabidhiwa, ukilinganisha na awali wakati ilipokuwa ikiendeshwa na BAKWATA.

Akitaja baadhi ya mafanikio hayo katika Taarifa fupi ya Shule hiyo kwenye mahafali ya kuwaaga Kidato cha NNE mwaka huu, yaliyofanyika Shuleni Mwishoni mwa wiki, Makamu wa Shule Ustadhi Fuadi Iddi amesema kuwa Shule imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka, kupitia jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Shule, walimu pamoja na wanafunzi, Kwa kuwapatia mazoezi ya kutosha, kutunza nidhamu ya Wanafunzi Kwa kuchukua hatua stahiki pale yanapotokea makosa, huku akiongeza kuwa kwa Kidato cha Nne wanaohitimu Mwaka huu, matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa, Shule ilipata Division one (10), D.II (35), D.III (21), D.IV (2), Zero (0). na shule ilishika nafasi 3/22 Kiwilaya na 13/171 Kimkoa.

Katika kuweka kando dhana ya Udini, Lilian Adriani, Kiiza Tugara, na Miriam Oscar ni miongoni mwa wahitimu wa Kidato cha Nne 2019 Kakangaga, mbali na mambo mengine wanaeleza wazi kuwa Mavazi ya Kujistiri, Taaluma na Maadili mema ndio sababu pekee zilizowashawishi kutoka shule zao za awali na kuhamia Kakangaga, hivyo na kuwepo kwao katika shule ya Kiislamu ilihali wao ni wakiristo, wamejifunza mambo mengi, yakiwemo Upendo, ushirikiano, na Umoja bila kubaguana.

 Pichani ni Wahitimu wa Kidato cha Nne Kakangaga Muslim Seminary, licha ya kuwa shule ni ya Kiislamu kimaadili lakini wao ni wakristo, kutoka kushoto ni Lilian Adrian, Kiiza Tugara na Miriam Oscar kama walivyokutwa na kamera yetu.
Pichani ni Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Kakangaga wakionekana na nyuso katika mahafali yao yaaliyofanyika Jumamosi hii shuleni Kakangaga Mkoani Kigoma.
 Pichani Baadhi ya Viongozi wa Dini kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Viongozi wa BAKWATA wamiliki wa Shule ya Kakangaga Muslim wakiwa meza Kuu katika mahafali ya kuhitimisha Kidato cha Nne kwa Mwaka wa Nane toka kuanzishwa shule hiyo.
 Pichani ni Mhitimu wa Kidato cha Nne Kakangaga Samir Haruna, ambae amekuwa Imam wa Shule toka Kidato cha Kwanza, akisoma Qur-an miongoni mwa Juzuu alizohifadhi, wakati wa mahafali yao ya kuhitimu Jumamosi hii.
 Pichani ni Mkuu wa Shule Kakangaga Muslim  Ustadh Abdul-Jalil Siraji Mustapha moja kati ya zao la Katoro Islamic Seminary, akitoa Salaam zake kwa Wazazi, walezi, na wanafunzi(hawapo pichani) wakati wa mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne 2019.



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35yiFJB
via

Post a Comment

0 Comments