MENEJA KLABU YA SIMBA ASIMULIA KIPIGO CHA MWADUI FC, AWEKA BAYANA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY, KAGERE NJE

  Masama Blog      
Kikosi cha Simba.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
BAADA ya kupokea kichapo cha goli moja kutoka kwa timu ya Mwadui FC ya Mjini Shinyanga, uongozi wa Klabu ya Simba umesema kwa sasa akili zote wamehamishia katika michezo inayofuata kwa kuanza na timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya.

Tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu Kikosi cha Simba kilikuwa hakijapoteza mchezo , hivyo Mwadui wamefanikiwa kushinda mchezo huo uliofanyika mkoani Shinyanga.

Akizungumza leo Novemba 1, 2019 jijini Dar es Salaam Meneja wa Klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema kuwa baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui wameelekeza nguvu zao katika mchezo wao na Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.

Amesisitiza kuwa wamejipanga na wachezaji wako fiti kukabiliana na Mbeya Citykwani wanachotaka ni kushnda mchezo huo na benchi la ufundi limejipanga vema. Hata hivyo amesema mshambuliaji wao Medie Kagere ataukosa mchezo dhidi ya Mbeya City kutokana na kuwa na kadi mbili za njano ikiwemo aliyoipata katika mchezo na Mwadui FC.

Kuhusu kufungwa na Mwadui FC, Meneja huyo wa Klabu ya Simba amesema hivi "Kwanza nieleze tu kufungwa na Mwanadui ni matokeo ya mchezo wa soka kama tunavyofahamu kuna kushinda, kufungwa au kutoka sare.Tumepoteza mchezo huo na ni matokeo ya mpira".

"Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri lakini kipindi cha pili hatukucheza kama inavyotakiwa licha ya kufanya mashambulizi ya mara kwa mara.Benji la ufundi litafanyia kazi maana wameshajua tatizo lilikuwa wapi,"amesema.

Alipoulizwa huenda Simba wamepoteza mchezo huo kutokana na ubovu wa kiwanja kilichotumika kwenye mchezo huo, Rweyemamu amejibu sababu sio kiwanja na kwamba viwanja karibu vyote nchini vinafafa na ndio viwanja vyetu."Kiwanja haikuwa tatizo, tusitafute sababu."

Ameongeza anachoweza kueleza spidi ya klabu ya Simba imepunguzwa sana kutokana na kufungwa na mwadui. Hata hivyo mpira ni mchezo wa kushangaza kwani usiyemdhania ndio huyo huyo anaweza kukufunga na ndicho ambacho kimetokea.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2pmd8GF
via
logoblog

Thanks for reading MENEJA KLABU YA SIMBA ASIMULIA KIPIGO CHA MWADUI FC, AWEKA BAYANA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY, KAGERE NJE

Previous
« Prev Post