Makatibu Tawala Wa Elimu Nchini Watakiwa Kuhakikisha Mashindano Ya KKKK Yanafanyika Kwa Ustadi

  Masama Blog      
Na, Editha Edward -Tabora .

Makatibu Tawala wasaidizi wa Elimu katika maeneo mbalimbali Nchini wametakiwa Kuhakikisha Mashindano ya Kusoma, kuandika, Kuhesabu na kuchora Yanafanyika kwa ustadi mkubwa kwa kuzingatia weledi na miongozo iliyotolewa na wizara ili kuleta matokeo chanya na hatimaye kupunguza kabisa idadi ya watoto wasiojua Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora

Akifungua Mashindano hayo ya Kusoma, kuandika Kuhesabu na kuchora Afisa Elimu mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora Msalika Makungu ametoa wito kwa wasimamizi wa Mashindano hayo kuzingatia weledi huku akibainisha kuwa Sherikali katika utekelezaji wa dira ya Taifa kuekekea uchumi wa kati ni muhimu watanzania kuweka mkazo katika utoaji wa stadi inayozingatia ujenzi wa stadi za msingi za ufundishaji na ujifunzaji

"Watahini wa kazi hii hakikisheni kuwa mnazingatia usawa na kuepuka upendeleo wakati wote mnapotekeleza majukumu yenu ili tuweze kupata wanafunzi mahiri watakaotuwakilisha vyema kitaifa"Amesema Nusu

Fatuma Shabani ni miongoni wa walimu waliopata mafunzo hayo amesema yatawasaidia kuwafundisha watoto kwa ueledi na ufanisi kwani wamepata uzoefu wa kutosha na maarifa

Aidha Mashindano hayo ya utambuzi yaliyojumuisha mikoa mitano Tabora , Simiyu, Singida Dodoma, na Shinyanga yatasaidia kuwaongezea ujuzi walimu lakini pia Ari katika utendaji wao wa kazi.
Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nusu ambaye amemuwakilisha katibu Tawala mkoa wa Tabora akitoa wito kwenye Mashindano hayo ya kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora
Wanafunzi wa shule ya za msingi mkoani Tabora waliohudhuria katika Mashindano hayo ya Kusoma kuandika Kuhesabu na kuchora.
Mwalimu akiwaelekeza wanafunzi waliohudhuria kwenye Mashindano hayo kwa michoro


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NYXmL0
via
logoblog

Thanks for reading Makatibu Tawala Wa Elimu Nchini Watakiwa Kuhakikisha Mashindano Ya KKKK Yanafanyika Kwa Ustadi

Previous
« Prev Post